Baada ya wapinzani wao wa jadi FC Barcelona kufanikiwa kuibuka na ushindi wa goli 3-0 dhidi ya River Plate ya Argentina katika fainali ya Klabu Bingwa Dunia, Real Madrid wameamishia hasira zao katika mchezo wa Ligi Kuu Hispania dhidi ya klabu ya Rayo Vallecano.
Real Madrid walikuwa katika dimba lao la nyumbani la Santiago Bernabeu huku timu yao ikiwa imesheheni mastaa wao kama Karim Benzema, Cristiano Ronaldo na Gareth Bale. Real Madrid wamefanikiwa kuibuka na ushindi wa goli 10-2 wakati Gareth Bale na Benzema wakiambulia kufunga hat-trick.
Magoli ya Real Madrid yalianza kufungwa dakika ya 3 na Danilo, Gareth Bale dakika ya 25, 42, 61 na 70, Cristiano Ronaldo dakika ya 30 na 54 na Karim Benzema dakika ya 48, 80 na 90. Wakati magoli ya Rayo Vallecano yalifungwa na Antonio Amaya dakika ya 10 na Jozabed dakika ya 12.
0 comments:
Post a Comment