Ikiwa saa kadhaa zilizopita FC Barcelona wamemaliza kucheza mchezo wao wa Copa del Rey dhidi ya Villanovense katika uwanja wao wa Nou Camp na kuibuka na ushindi mnono wa goli 6-1, wapinzani wao wa jadi Real Madrid walishuka dimbani saa kadhaa mbele kucheza dhidi ya Cadiz ugenini.
Real Madrid ambao hali ya maelewano ya kocha wao Rafael Benitez na staa wa timu hiyo Cristiano Ronaldo inatajwa
kuwa ndogo, walishuka dimbani kucheza mchezo huo na kufanikiwa kuibuka
na ushindi wa goli 3-1 licha ya kuwa katika uwanja wa ugenini, Real Madrid walitumia dakika 3 za mwanzo kupachika goli la kwanza kupia kwa Denis Cheryshev.
Licha ya kuwa Cadiz ni timu ndogo na haishiriki Laliga ila inacheza Segunda, iliwasumbua Real Madrid na kuwafanya wachelewe kupata magoli mengi zaidi hadi pale Isco alipofunga goli mbili za haraka dakika ya 66 na 74, huo haukuwa mwisho wa Cadiz kuwashambulia Real Madrid kwani dakika ya 88 Kike Marquez akafunga goli la kufutia machozi kwa Cadiz.
Video ya magoli ya Cadiz Vs Real Madrid
0 comments:
Post a Comment