Mwenyekiti
wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji Mstaafu Damian Lubuva (kulia)
akizungumza na waandishi wa habari (ambao hawapo pichani) leo jijini Dar
es Salaam kuhusu uchaguzi wa wabunge unaotarajiwa kufanyika Tarehe
13/12/2015 katika jimbo Handeni na Arusha Mjini,(kushoto) ni Kaimu
Mkurugenzi Idara ya Habari na Elimu ya Mpiga Kura Bw.Clarence Nanyaro
kutoka Tume ya Taifa ya Uchaguzi.
Baadhi
ya waandishi wa habari wakimsikiliza Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya
Uchaguzi Jaji Mstaafu Damian Lubuva(ambaye hayupo katika picha) leo
jijini Dar es Salaam alipokuwa akizungumza na waaandishi wa habari
kuhusu taratibu zitakazo tumika katika uchaguzi wa wabunge katika jimbo
la Arusha na Handeni.
Tume
ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imetangaza siku ya kupiga kura kwa baadhi ya
majimbo ambayo uchaguzi wake ulihairishwa kutokana na sababu mbalimbali
Akiongea
na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam, Jaji Mstaafu Damian
Lubuva ametaja siku hiyo ya uchaguzi itakuwa Disemba 13, mwaka huu.
“Natoa
rai kwa Wananchi wote waliojiandikisha kama wapiga kura katika Majimbo
na Kata husika kujitokeza katika vituo walivyojiandikishia ili kuweza
kupiga kura na kuwachagua viongozi wanaowataka” amesema Lubuva.
Jaji
Lubuva aliyataja majimbo hayo ambayo wananchi watapiga kura za kuchagua
Wabunge kuwa ni Majimbo ya Arusha Mjini na Handeni Mjini ambapo
uchaguzi wa Madiwani katika kata za Mvomero, Ipala na Nyamwilolewa nao utafanyika siku hiyo.
Aidha, Jaji Lubuva alisisitiza
kuwa, taratibu zilizotumika katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 25, 2015
mwaka ndizo zitakazotumika kwenye uchaguzi kwenye majimbo hayo na kata
hizo.
Kwa
ufupi, Jaji Lubuva alikumbushia baadhi ya taratibu hizo zikiwemo za
mpiga kura kubeba kadi yake ya kupigia kura pindi aendapo kupiga kura,
mawakala wa vyama vya siasa lazima wawepo kwenye kila kituo na pia
Maafisa Uchaguzi kufungua kituo na kufunga kwa muda uliopangwa na Tume.
Katika Uchaguzi Mkuu uliofanyika tarehe 25 Oktoba 2015, uchaguzi wa Wabunge na Madiwani wa Majimbo 7 pamoja na Kata 35 ulihairishwa kutokana na sababu mbalimbali zikiwemo za vifo na vurugu.
0 comments:
Post a Comment