Hii inakuwa mara ya pili kukutana na taarifa ya ziara ya ghafla iliyofanywa na Waziri Mkuu mpya wa Tanzania, Majaliwa Kassim Majaliwa…
mara ya kwanza ilikuwa siku chache zilizopita ambapo aligundua upotevu
wa makontena 349, watu 12 wakakamatwa na Jeshi la Polisi kwa ajili ya
uchunguzi.
Kituo cha ITV kimeripoti kuwa Waziri Mkuu huyo amefanya tena ziara ya ghafla bandarini Dar pamoja na Shirika la Reli TRL na kubaini ubadhirifu mwingine, ya leo inahusu upotevu wa makontena mengine 2431 !!
Naifatilia hii kwa ukaribu, chochote kitakachonifikia nitakufikishia wakati wowote !!
0 comments:
Post a Comment