Baada Ya "My God Is Gudoooo", Sasa Ni "I go Shout I go Dansoooo" Ya Uche Yazidi Kuchukua Kasi.
Mwanamuziki Mwenye Asili ya Nigeria anayefanya kazi za Muziki South Africa Na Marekani Pastor Uche Agu, Maarufu kwa Jina la "Double Double" ambaye katika Albam ya 14 Ya Joyous Celebration aliimba wimbo wa My God Is Gudooo, na Kuwa Maarufu Wimbo huo ndani na Nje ya bara la Africa, na baadae katika Albam ya 15 ya Joyous Celebration kuimba wimbo Wa Solid Rock, Safari hii Wimbo wake wa Kwenye Albam Ya 16 Ya Joyous Celebration wenye Kibwagizo cha 'I go Shout I go Dancooo" kimeanza kushika kasi yake. Mpaka Sasa Pastor Uche Agu ameshashiriki Kuimba Joyous Celebration Albams 4, kuanzia JC 13 mpaka sasa ya 16.
Katika Albam ya Joyous Celebration 16, Uche ameimba wimbo wenye jina la Overflow ambapo moja ya vibwagizo katika ni hizo Lafudhi za Kinegeria za 'I go Shout. I go Dansoooo". Katika Conversation ya Blog iliyofanywa na wadau mbalimbali ndani na nje ya bara hili kupitia Mtandao wa Facebook, unaonesha Urahisi wa Maneno ya Wimbo Huo Umeufanya utumike zaidi katika "Praise".
Mdau wa blog Kutoka South Africa Mwenye asili ya Kitanzania ameeleza "WOZA Dancing Ya Uche ndiyo imekuwa Style ya Vijana Katika Praise". Katika Albam hiyo Ya 16 Uche ameonesha ubunifu wake kwenye style ya Kucheza ya hamasa South Africa almaarufu "WOZA".
Twende sawa utazame, Style ya WOZA ya UCHE katika Kucheza na pia "I go Shout, I go Dansoo"
0 comments:
Post a Comment