ANGALIA PICHA ZA TUKIO LA TUZO ZA AFRICA GOSPEL MUSIC AWARDS 2012
Siku ya jumamosi jijini London nchini Uingereza kumefanyika tukio kubwa
la utolewaji wa tuzo za Africa Gospel Music Awards(AGMA) 2012, tukio
hilo ambalo watanzania wengi walikuwa na matarajio ya kuona mwimbaji wao
pekee aliyependekezwa kuwania tuzo hizo katika vipengele viwili
kushindwa kupata tuzo hizo kutokana na kura alizopigiwa kuwa chache
hivyo kuwapa mwanya waimbaji wengine aliokuwa akiwania tuzo hizo
kuondoka na tuzo hizo, bofya hapa kujua washindi.
Onyesho hilo ambalo lilianza kwa kupooza kutokana na watu kuchelewa
kuanza kuingia ukumbini pia asilimia kubwa ya watu hata walipoingia
ukumbi huo ulio chini ya El shaddai Christian Centre waimbaji waliokuwa
wakiimba hawakuweza kuwafanya watu hao wasimame zaidi ya kufurahia
huduma yao kwa kuwapigia makofi mara walipomaliza kuimba. Shughuli hiyo
ambayo iliongozwa na washereheshaji (MC) wapatao wanne wakiwemo waimbaji
kama Diana Hamilton, Rebecca, Wole Awola na mwenzao ambaye ni
mchekeshaji aliyeweza kuwavunja mbavu kwa vicheko kutokana na lafudhi na
vichekesho hivyo kuwahusu hasa watu kutoka Afrika magharibi ambao
walikuwa wameujaza ukumbi huo.
Mwanadada Emmy Kosgei kutoka nchini Kenya ambaye usiku huo alijishindia
wimbo bora wa mwaka ndiye aliweza kusimamisha watu waliokuwepo ukumbini
hapo kwa jinsi alivyoweza kuimba kwa ustadi nyimbo zake mbili ukiwemo
Ololo ambazo kila wimbo aliimba kwanza kwa CD kisha wanamuziki
waliokuwepo kuendeleza live mara ulipoisha kwakuwa hawakuweza kufanya
mazoezi kabla, mwimbaji huyo aliweza kuwa nyota usiku huo kwani baada ya
tamasha nusu ya watu walioujaza ukumbi huo walimzunguka kutaka kupiga
picha naye pamoja na kuchukua mawasiliano yake.
Kundi la Makoma ambalo halikuweza kupata tuzo yoyote usiku huo
halikuweza kufika ukumbini hapo kwa wakati kutokana na taarifa
zilizopatikana baadaye kwamba walipata ajali wakiwa njiani kuja ukumbini
hapo ndio maana hawakufika ingawa walituma meneja wao pamoja na mmoja
wa waimbaji wa kundi hilo ambaye alipozungumza na GK akasema Makoma wapo
vizuri, Mungu akipenda wanapanga kuja Tanzania mwakani
.
NJE YA UKUMBI TUZO ZILIPOTOLEWA |
HAPA NI MWONEKANO WA UKUMBI KWA NDANI |
HAYA NDIYO MAJINA YA WASHINDI AGMA TUZO ZILIZOTOLEWA NCHINI LONDON
PAMOJA NA CATEGORIES ZAO
AGMA 2012 WINNERS
EVENT OF THE YEAR SPONSORED BY EAGLE ENTERTAINMENT
Joyous Celebration 16 Live Recording (South Africa)
RADIO PROGRAM OF THE YEAR SPONSORED BY LONDON CHRISTIAN RADIO
Indumiso- Ukozi FM
RADIO PRESENTER OF THE YEAR SPONSORED BY VOICE OF AFRICA RADIO
Anthony Ndiema- Kenya Fiifi Folson- Ghana
TV CHANNEL/ PROGRAM OF THE YEAR SPONSORED BY FAITH TV
One Gospel (South Africa)
TV PRESENTER OF THE YEAR SPONSORED BY OHTV Shoggy
Tosh
DISCOVERY OF THE YEAR SPONSORED BY G FORCE RADIO
PK Boadi-UK Prosper Mateva -Zimbabwe
AFRO JAZZ/ INSTRUMENTAL MUSICIAN OF THE YEAR SPONSORED BY AFROLINK Mike Aremu (Nigeria)
AFROGOSPEL RAP ARTISTE/GROUP OF THE YEAR SPONSORED BY KEEP THE FAITH MAGAZINE
Rooftop MCs (Nigeria) Andrew Bello (UK)
ARTISTE OF THE YEAR EAST AFRICA
Dawit Getachew- Ethiopia
ARTISTE OF THE YEAR WEST AFRICA SPONSORED BY MONEYGRAM
Frank Edwards-Nigeria
ARTISTE OF THE YEAR CENTRAL AFRICA SPONSORED BC3 MEDIA
Mike Kalambayi (Congo)
ARTISTE OF THE YEAR SOUTHERN AFRICA SPONSORED BY CONSTANCE BANQUET
Patrick Duncan
ARTISTE OF THE YEAR USA/CANADA SPONSORED BY MISS TEE
Yaw Osei-Owusu
ARTISTE OF THE YEAR AUSTRALIA/ASIA SPONSORED EAGLE ENTERTAINMENT
Disciple
ARTISTE OF THE YEAR EUROPE SPONSORED MEDIA MIND
Rebecca,
UK MUSIC PRODUCER OF THE YEAR SPONSORED BY PAULINE LONG BEFFTA
Wole Oni - (Nigeria) Billy Frank (Kenya)
GROUP/CHOIR OF THE YEAR SPONSORED BY Simply Chrysolite-South Africa
VIDEO OF THE YEAR
God Dey Bless Me- Cwesi Oteng – Ghana
SONG OF THE YEAR SPONSORED BY LYCA MOBILE
Ololo – Emmy Kosgei (Kenya)
ALBUM OF THE YEAR SPONSORED PREMIER GOSPEL
Colours of Africa- Sonnie Badu
(UK) FEMALE ARTISTE OF THE YEAR
Lara George- Nigeria
MALE ARTISTE OF THE YEAR
Solly Mahlangu-South Africa
AGMA SPECIAL AWARDS BEST CONTRIBUTION TO THE PROMOTION OF AFRICAN GOSPEL MUSIC
Voice of Africa Radio
Bola Mogaji Wole Oni
Premier Gospel BC3 Media
Jabu Hlongwane
John Mensah Sarpong
AGMA TRAILBLAZER AWARD
Sammie Okposo
Sonnie Badu Muyiwa Olarewaju
LIFETIME ACHIEVEMENT AWARD
Rev. Benjamin Dub
0 comments:
Post a Comment