bondia francis cheka katika pozi |
Novemba 9, 1996 mabondia wawili wa Kimarekani
wa uzito wa juu waliokuwa na majina
makubwa ulimwenguni Evander Holyfield
na Make Tyson, walisababisha kuibuka hisia za udini katika pambano lao na hivyo waliwagawa wapenzi wa ngumi
katika makundi mawili ya Kikristo na Kiislamu, kufuatia Tyson kuamua kusilimu
na kujitangaza kuwa mfuasi wa dini hiyo
kupitia Allah na Mjumbe wake Mtume Muhammad (SAW).
Wakati wa pambano lao lililofanyika katika ukumbi wa MGM Grand
Garden Arena ulioko Jijini Las Vagas Jimboni Nevada nchini Marekani bondia
Holyfield aliyejitangaza kuwa mlokole anayemuamini Mungu Yehova kupitia mwanaye
Yesu Kristo, aliingia ulingoni huku amevali vazi lenye ujumbe unaotoka katika
kitabu cha Wafilipi 4:13, akitamba kumsambaratisha vibaya Tyson ambaye alikuwa
na sifa ya kushinda mapambano yote, ambapo alifanikiwa kumpiga vibaya mwishoni
mwa round ya 10.
Kabla na baada ya
kupigana na Tyson na kumshinda kwa kishindo, alipohojiwa na Vyombo vya Habari
Holyfiel alinukuliwa akisema kwa msisitizo kwamba alikuwa na uhakika wa
kushinda kutokana na Roho Mtakatifu kumhakikishia hilo.
Bondia Tyson alisambaratishwa ulingoni na Mlokole Holyfield katika round hiyo ya 10 ya pambano
lililogubikwa na hisia za kidini, ikiwa ni muda mfupi baada ya kusilimu, ambapo umaarufu wake
ulishuka vibaya na kujikuta akipoteza takribani mapambano
yote yaliyofuata hadi alipostaafu ngumi.
Pambano hilo hadi leo lilimecha utafsiri kwamba siku zote anayemuamini Yesu ni mshindi na kwamba wakati
mwingine Mungu Yehova anaweza kuonesha ukuu wake katika njia ambazo binadamu
anaweza kuona kama vile zina utata,
lakini bado akaendelea kuitwa Mungu mwenye haki na rehema.Askofu Zakaria Kakobe wa Full Gospel Bible Fellowship |
0 comments:
Post a Comment