Home » »

MWIMBAJI WA JOYOUS KUWA MWEUSI WA KWANZA KUSHINDA SA IDOLS MWAKA HUU AFRIKA YA KUSINI?

Rising Star, Khaya Mthethwa
Khaya alipoimba wimbo uliompa tiketi ya kuingia 16 bora.
Kijana anayekuja kwa kasi ya ajabu katika medani ya muziki nchini Afrika ya kusini ambaye ameingia kwenye kinyang'anyiro cha SA IDOLS Season 8 aitwaye Khaya Mthethwa anatajwa sana kwenye vyombo vya habari nchini humo kwamba moto anaouonyesha sasa katika shindano hilo kama ataendelea nao, basi hakuna ubishi atakuwa mtu mweusi wa kwanza kushinda shindano la SA Idols mwaka huu.

Kijana huyo ambaye yupo kwenye top 16 mpaka sasa anaonekana kutajwa sana midomoni mwa watu pamoja na watangazaji wa vyombo vya habari, wiki iliyopita alipata sapoti kubwa baada ya waimbaji wenzake wa kundi la Joyous Celebration walipoamua kutinga ukumbi walipokuwa wakiperfom washindanaji hao huko Soweto ikiwa ni moja ya ratiba ya waendeshaji wa shindano hilo kwa waimbaji kuimba kwenye moja ya ukumbi na watu kuwashuhudia. Ambapo waimbaji wa Joyous na mashabiki wa kundi hilo kwa pamoja wanaendesha kampeni ya kuhakikisha mwimbaji huyo anashinda kwenye shindano hilo.

Mwimbaji huyo ameonekena katika toleo la 15 na la 16 la Joyous akiwa amefanya kazi kubwa yakupendeza, licha ya mashabiki wa kundi hilo kumuombea na kumpigia kura ili ashinde, tayari wameonyesha wasiwasi kwamba ndio utakuwa mwisho wake wa kuimba ndani ya Joyous, kutokana na hilo mashabiki wanaliomba kundi hilo kuhakikisha kwamba wanaambatana na mwimbaji huyo katika show za kundi hilo zinazotarajia kufanyika mwezi katika ukumbi wa ICC Durban, ambako ndiko anakotokea mwimbaji huyo.


                                         Photo: Team Khaya!! Please Family n Friends Support Him......
Facebook Blogger Plugin: Bloggerized by Joseph Kipangula Enhanced by Joseph Kipangula

0 comments:

Post a Comment

NURU FM 93.5 IRINGA

.

.

.

Nyali

Pages

Pages

Powered by Blogger.

Blog Archive

Search This Blog