HIVI NDIVYO SHUGHULI ZA UOKOAJI VILIVYOENDELEA KWA ABIRIA WA AJALI YA MELI
Mwokoaji akiwa na mmoja wa maiti wa ajali hiyo
Waokoaji wakiokoa moja ya maiti. wakiwa katika boti ya Kilimanjaro.
Majeruhi wakiwa katika mgongo wa boti hiyo wakisubiri kuokolewa.
Baadhi ya Abiria wakiwa katika moja ya chombo cha kuokolea wakielea baharini wakisubiri kuokolewa.
Boti ya KMKM ikiwa katika zoezi la kuokowa majeruhi.
Majeruhi alieokolewa katika meli ya Star Gate iliozama huko katika bahari ya Chumbe Zanzibar na ikiwa na abiria 250. Picha/Ramadhan Othman Ikulu
Daktari akitowa huduma ya kwanza kwa mmoja wa majeruhi wa boti iliozama ikiktokea Dar-es-Salaam kuelekea Zanzibar
Majeruhi wa ajali ya Meli wakiwa katika Hospitali ya Mnazi Mmoja wakipata huduma baada ya kuokolewa.
Majeruhi wakiwa katika hospitali ya Mnazi Mmoja
Picha ziadi maafa ya meli
Watalii na raia wa kigeni pia walikuwemo katika meli iliyozama hawa ni baadhi ya waliosalimika
Abiria waliookolewa kutoka katika meli iliozama ya Star Gate katika bahari ya Chumbe Zanzibar
Abiria aliyeokoka kutoka katika meli iliyozama
Abiria
aliyookoka katika Meli iliozama ya Star Gate akifarijiwa na Jamaa zake
Baada ya kuteremka katika Meli iliowaokoa hapo Bandarini(Bofya hapa
HUKu kukiwa bado na tarifa zenye utata juu ya idadi kamili ya waliokufa katika ajali ya meli huko Zanzibar ,mamlaka ya Udhibiti Usafiri wa Nchi Kavu na Majini (SUMATRA) imesema, meli iliyozama leo, katika kisiwa cha Chumbe, Zanzibar ilikuwa na abiria 248 wakiwemo watoto 31.
HUKu kukiwa bado na tarifa zenye utata juu ya idadi kamili ya waliokufa katika ajali ya meli huko Zanzibar ,mamlaka ya Udhibiti Usafiri wa Nchi Kavu na Majini (SUMATRA) imesema, meli iliyozama leo, katika kisiwa cha Chumbe, Zanzibar ilikuwa na abiria 248 wakiwemo watoto 31.
Taarifa ya
mamlaka hiyo hiyo imesema, meli hiyo, Mv Skagit iliondoka katika
Bandari ya Dar es Salaam leo saa sita mchana, ikiwa na mabaharia tisa.
Kwa
mujibu wa Sumatra, meli hiyo, inamilikiwa na Kampuni Seagul Transport,
imasajiliwa na Mamlaka ya Usafiri Baharini Zanzibar (ZMA) na kwamba,
Cheti cha Ubora kimeanza tarehe 24 Agosti, 2011 na kinamalizika 23
Agosti, 2012. Imesema, meli hiyo ilikuwa imeruhusiwa kubeba abiria
wanaoruhusiwa 300 na tani 26 za mizigo.
“SUMATRA
kupitia Kituo cha Utafutaji na Uokoaji (MRCC) ilipata taarifa kuwa
meli ya MV Skagit iliyokuwa safarini kutoka Dar es Salaam kuelekea
Zanzibar ilikuwa inazama katika eneo la karibu na kisiwa cha Chumbe,
Zanzibar, eneo ambalo lipo umbali wa Kilomita za Bahari 13.8 kutoka
Bandari ya Zanzibar” imesema taarifa hiyo.
Kwa
mujibu wa Sumatra, baada ya kupata taarifa hizo, kituo cha MRCC
kilitoa taarifa kwa vyombo vya ulinzi na usalama pamoja na vyombo vya
usafiri wa majini vilivyokuwa karibu na eneo la tukio.
“
Zoezi la uokoaji linaendelea katika eneo la tukio kwa msaada wa vyombo
vifuatavyo: Mv Flying Horse, Mv Kilimanjaro III, Tug Bandari ya
Zanzibar, KMKM, Mv Zanzibar I, Police Patrol Boat, Navy” imesema
taarifa hiyo.
0 comments:
Post a Comment