MWANDISHI WAPO RADIO KUAGWA LEO KIJICHI
Mwili wa mtangazaji na muandaaji msaidizi wa Michezo wa WAPO Radio FM,
Joseph Pancras Mapunda utaagwa leo nyumbani kwake Mtoni Kijichi -
Bujonga kuanzia saa nane mchana, baada ya kufanyika ibada. Ratiba nzima
ya shughuli iko kama ifuatavyo.
Saa 5 - 6:00 Mchana - Chakula Nyumbani kwa Marehemu
Saa 6 - 7:00 Mchana - Mwili wa marehemu kuwasili nyumbani
Saa 7 - 8:00 Mchana - Ibada - nyumbani kwa marehemu
Saa 8 - 9:00 Mchana - Kuaga mwili wa marehemu
Saa 9 -10:00 Alasiri - Safari ya kwenda kuupumzisha mwili (makaburi ya Chang'ombe maduka mawili)
Saa 10 Jioni - Ibada - (makaburi ya Chang'ombe maduka
mawili) Hapa ndipo itakuwa mwisho wa safari ya mpendwa wetu Joseph
Mapunda.
Jinsi ya kufika nyumbani kwa marehemu, panda magari ya Mtoni Kijichi au Mbagala Kuu, shuka kituo cha mwisho (CCM) hapo utatembea kama mita mia moja, kuna kituo kinaitwa Zahanati, hapo kuina transfoma kubwa, utakata kona mkono wa kulia, na hapo utakuwa umefika maeneo ya msibani. (kwa Bujonga)
Joseph Mapunda, pia amekuwa kocha wa timu ya WAPO FC kipindi cha uhai wake. |
Kwa wale wanaopenda kushiriki rambirambi, wanaweza kufika WAPO Radio FM
na kuonana na Joyce Matthew, ama kwa walio mbali, wanaweza kushiriki kwa
kutuma mchango wao kupitia tiGO Pesa na M-Pesa kwa namba 0717-572-066
na 0767-572-066.
Joseph Pancras Mapunda, ama kwa jina la utani 'BABU' kama ambavyo
amekuwa akiitwa na wanamichezo wenzake WAPO Radio FM, amefariki siku ya
jumamosi katika hospitali ya wilaya ya Temeke alipokuwa amelazwa kuanzia
alhamisi usiku. kesho yake ijumaa - alikuwa kwenye matibabu, lakini
ilipofika jumamosi, ambapo wafanyakazi wenzake walikwenda kumjulia hali
baada yakuwa na kikao, ndipo wakakuta mapazia ya kijani yamezungushiwa
kwenye kitanda cha Joseph. Madaktari wanasema, Joseph alikuwa na uvimbe
tumboni, ndio uliopelekea kumchukua.
Mshtuko ulikuwa mkubwa, uliojawa na hofu - Joseph Mapunda
alikwishatangulia, na kuacha mjane na watoto wawili, ambao bao ni
wanafunzi shule ya msingi.
Bwana ametoa, na Bwana ametwaa, jina la Bwana lihimidiwe.
0 comments:
Post a Comment