Mwimbaji wa kundi la The Voice linaloundwa na vijana watano aitwaye
Obedi John Mark amepata ajali jana usiku majira ya saa tatu maeneo ya
Sinza Kamanyola, akiwa anatumia usafiri wa bajaji. kupitia ukurasa wao
wa Facebook kundi hilo limetoa ujumbe huu;-
''Mwimbaji mwenzetu Obedi
John Mark amepata ajali maeneo ya Sinza Kamanyola, akiwa na usafiri wa
bajaji akiwa anaelekea Magomeni...Kwa sasa hali yake si nzuri yuko chini
ya uangalizi wa Daktari Mvungi ndani ya Hopitali ya Kinondoni na
ameumia sehemu za Kichwa, wapendwa tuzidi kumuombea apone haraka''.
|
Obedi Mark katika pozi. |
Aidha mwana blogger mwingine unlce jimmytemu kupitia blog
yake amefanya mazungumzo na mdogo wake Obedi nakueleza kuwa hali yake
sio nzuri amepata michubuko kwenye Mikono Miguu na sehemu za uti wa
mgongo.Kwa sasa yupo hospital Muhimbili.
Gospel Kitaa inamtakia afya njema Obedi Mungu ahusike katika matibabu
yake, tungependa kumuona akijumuika na wenzake katika huduma ya kumwinua
Kristo.AMEN
|
The Voice. |
0 comments:
Post a Comment