HUDUMA YA OVERCOMERS POWER CENTER YA MJINI IRINGA CHINI YA DR.BISHOP BOAZ SOLLO YAZINDUA OPERATION YA SAFISHA UCHAWI  NA NGUVU ZA GIZA KUANZIA ALHAMISI 20 MARCH HADI PASAKA.
Akizungumza na mtandao huu askofu boaz sollo amesema msako huo unakuja baada ya kuona watu wengi wanaonewa sana na shetani hivyo ametoa wito kwa watu wote kuungana nae katika kuvunja na kubomoa ngome zote za shetani ambaye amekuwa akiwatumikisha watu.
uzinduzi wa operation hiyo utafanyika katika ukumbi wa huduma hiyo unaoendelea kujengwa katika mtaa wa zizi la ng'ombe ambapo hadi sasa ukumbi wa awali unatarajiwa kukamilika muda wowote kuanzia sasa
askofu boaz sollo ambaye pia ni mkurugenzi wa kituo cha redio mkoani iringa ameendelea kufanyika baraka kwa wakazi wa mikoa ya nyanda za juu kusini pamoja na kati ambao wamekuwa wakimshukuru kwa jinsi ambavyo mungu amekuwa akimtumia kwa viwango vya hali ya juu.
          zifuatazo ni picha za makitaba
[Image]

[Image]
.
[Image]

KANISA LA WINNERS CHAPEL LA MAMILIONI LIPO KATIKA HATI HATI YA KUBOMOLEWA NA SERIKALI

[Image]
Winners Chapel la jijini Nairobi muonekano wa ndani.
Kanisa kubwa la kisasa la Winners Chapel la jijini Nairobi nchini Kenya liko kwenye hati hati ya kubomolewa na serikali ya nchi hiyo, kwa madai ya kiwanja lilipojengwa kanisa hilo ni mali ya serikali na kwamba kanisa hilo lilifanya makosa kujengwa mahali hapo.

Kanisa hilo lenye uwezo wa kubeba waumini elfu kumi na wanane (18,000) kwa wakati mmoja ambalo ujenzi wake umechukua miaka tisa hadi kukamilika kwake likiwa limejengwa eneo la south B estate huku likitajwa kuwa ni moja kati ya makanisa bora kujengwa Afrika mashariki na kati liko chini ya kanisa mama la Winners Chapel lenye makao makuu yake nchini Nigeria chini ya kiongozi na mwanzilishi wake mchungaji David Oyedepo anayetajwa kuwa mmoja kati ya watumishi wa Mungu matajiri duniani.

[Image]
Winners Chapel la jijini Nairobi nchini Kenya, katika muonekano wa nje.©skyscrapercity
Kwa mujibu wa vyanzo mbalimbali vya habari vya nchini Kenya vinasema kwamba katibu mkuu wa kilimo, ufugaji na uvuvi wa kenya bwana Felix Kosgey amesema serikali itatoa siku 21 kwa wamiliki wa nyumba hizo katika kiwanja cha diamond park ambacho kimejengwa nyumba mbalimbali za kifahari pamoja na south B ambako kumejengwa kanisa hilo kuondoka ili zibomolewe tayari kwa matumizi mengine ya serikali.

Kiwanja hicho chenye jumla ya ekari 210 kimezua mzozo na kufikia wakazi wake kufika ofisini kwa meneja mradi wa nyumba hizo Ahmed Rashid ili kupata ufafanuzi juu ya kauli iliyotolewa na bwana Kosgey. Ambapo kwa mujibu wake meneja huyo amesema toka kutolewa kwa kauli hiyo wamekuwa katika wakati mgumu kutoka kwa watu hao na wengine wakipiga simu kutoka nje ya nchi wakiulizia uhalali wa eneo hilo ambalo amesema lina nyumba zipatazo 600 ambazo zipo katika eneo hilo kwa miaka 10 sasa huku kila nyumba ikiwa inathamani ya shilingi milioni 16 za Kenya huku wengine wakiwa wamiliki na wengine wapangaji katika nyumba hizo.

[Image]
Mchungaji Oyedepo katikati na mkewe sambamba na makamu wa Rais wa Kenya bwana William Ruto wakikata keki wakati wa uzinduzi wa kanisa hilo ambalo lipo katika hatihati ya kubomolewa.©gadiola25
Kwa upande wa mmoja wa wachungaji wa kanisa la Winners ambaye hakupenda jina lake litajwe kwakuwa si msemaji wa kanisa ameiambia Nairobi news kwamba kabla hawajaanza ujenzi wa kanisa hilo waliwakilisha nyaraka zote muhimu kwa vyombo husika.




[Image]
Nyumba ambazo zipo katika hatihati ya kubomolewa katika eneo la Diamond Park jijini Nairobi ©nairobinews
[Image]
Moja ya ndege ya kifahari ya kiongozi wa kanisa la Winners duniani David Oyedepo.©dailymail
[Image]
Mchungaji David Oyedepo akiwa ndani ya ndege yake, akifurahia jambo.©dailymail

UZINDUZI WA KAMPENI ZA UCHAGUZI MDOGO WA UBUNGE CHALINZE WAFANA

2Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Ndugu Abdulrahman Kinana akiwahutubia wananchi wa jimbo la Chalinze katika mkutano wa hadhara uliofanyika mjini Chalinze leo.3Mgombea wa ubunge jimbo la Chalinze Bw. Ridhiwan Kikwete akiwahutubia wananchi wa jimbo la Chalinze wakati alipokuwa akiomba kura.4Mama Salma Kikwete Mke wa Rais na mjumbe wa Halimashauri kuu kutoka mkoa wa Lindi akimsikiliza mmoja wa waliokuwa wagombea wa jimbo la Chalinze katika mchujo ndani ya Chama cha Mapinduzi Ndugu Imani Madega mara baada ya kumuombea kura Rihiwani Kikwete, katikati ni Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Mh. Meck Sadik5mmoja wa waliokuwa wagombea wa jimbo la Chalinze katika mchujo ndani ya Chama cha Mapinduzi Ndugu Imani Madega kulia akizungumza na Ridhiwani Kikwete mara baada ya kumuombea kura6mmoja wa waliokuwa wagombea wa jimbo la Chalinze katika mchujo ndani ya Chama cha Mapinduzi Ndugu Imani Madega akimuombea kura Ridhiwani Kikwete.7Msaniki Sam wa Ukweli kushoto akiwa katika picha ya pamoja na mpenzi wa Chama cha Mapinduzi Bw. Mustafa Selemani.Mama Salma Kikwete Mke wa Rais na mjumbe wa Halimashauri kuu kutoka mkoa wa Lindi akiwahutubia wananchi katika mkutano huo.Mbunge wa Simanjiro Mh. Christopher Ole Sendeka akiwahutubia wananchi wa Chalinze wakati wa mkutano huo.Nape Nnauye Katibu wa Itikadi, Siasa na Uenezi akizungumza na kukaribisha baadhi ya viongozi katika mkutano huo.Mama Salma Kikwete Mke wa Rais na mjumbe wa Halimashauri kuu kutoka mkoa wa Lindi akimsikiliza mkuuu wa mkoa wa Dar es salaam Mh. Meck Sadik.Kundi la muziki la TOT likitumbuiza katika mkutano huo.

14Wananchi waliojitokeza katika mkutano huo wakiwa wamebeba Picha za mgombea ubunge wa jimbo hilo kupitia CCM Bw. Ridhiwani Kikwete.15Malkia wa muziki wa Taarab kutoka kundi la TOT Khadija Omar Kopa kulia akiongoza kundi hilo wakati lililpokuwa likitumbiza katika mkutano huo leo.16Marafiki mbalimbali wa mgombea ubunge wa jimbo la Chalinze kupitia CCM Bw. Ridhiwani Kikwete waliojitokeza katika mkutano huo  wakinyanyua juujuu mabango yenye picha zaRidhiwani Kikwete.17Cheki hili nyomi18Mama Salma Kikwete Mke wa Rais na mjumbe wa Halimashauri kuu kutoka mkoa wa Lindi kulia, Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana katikati na mgombea ubunge wa jimbo la Chalinze kupitia CCM Ndugu Ridhiwani Kikwete wakiondoka eneo la Mkutano mara baada ya kumalizika.19Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana katikati, Nape Nnauye Katibu wa Itikadi, Siasa na Uenezi na Ridhiwani Kikwete wakitembea kwa miguu kuelekea eneo la mkutano uliofanyika viwanja vya Polizi mjini Chalinze leo.





WAHITIMU KUTOKA SHULE MBALIMBALI KUTOKA MANISPAA YA IRINGA WAKIIMBA WIMBO WA PAMOJA.





               Naomi kutoka shule ya wasichana iringa akiiimbisha wimbo kwa makini
                                       endelea kufuatilia habari picha

MAHAFARI YA KIDATO CHA SITA P.S.A MANISPAA YA IRINGA YAFANA


      Mchungaji mlezi wa mkoa pamoja na mgeni rsmi madamu recho wakijiandaa kuingia ukumbini.

NURU FM 93.5 IRINGA

.

.

.

Nyali

Pages

Pages

Powered by Blogger.

Search This Blog