Ikiwa ndani ya wiki zisizo pungua tatu
ulimwengu wa soka umepokea taarifa za vifo vya wanasoka wawili, mchezaji
wa timu ya taifa ya Honduras Arnold Peralta na aliyekuwa mchezaji wa zamani wa timu ya taifa ya El Salvador Alfred Pacheco. January 2 ulimwengu wa soka umepokea taarifa za kifo cha beki wa zamani wa timu ya taifa ya Ivory Coast na klabu ya Wigan Athletic Steve Gohouri.
Steve Gohouri ambaye alikuwa mahiri katika nafasi ya beki amekutwa amefariki katika mto Rhine wa Ujerumani,
taarifa ambazo zimetoka ikiwa alipotea kwa muda wa wiki mbili, pasipo
kujulikana wapi alipo, wiki mbili zilizopita aliripotiwa kupotea na
kutafutawa bila mafanikio hadi January 2 mwili wake ulipokutwa mto Rhine.
Staa huyo ambaye amefariki akiwa na umri wa miaka 34, aliwahi kuichezea klabu ya Wigan Athletic ya Uingereza kuanzia mwaka 2010 hadi mwaka 2012, lakini amechezea timu yake ya taifa ya Ivory Coast toka mwaka 2006 hadi mwaka 2011 ndio alianza kukosekana timu ya taifa.
0 comments:
Post a Comment