Waziri
Mkuu Kassim Majaliwa amekagua maghala ya Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya
Chakula (NFRA) kanda ya Songea, wakati akiendelea na ziara yake mkoani
Ruvuma.
Akizungumza
na wafanyakazi wa Wakala hiyo, wadau wa kilimo pamoja na wananchi jana,
(Jumatatu, Januari 4, 2016) nje ya majengo ya Wakala mara baada ya
kukagua mahindi yaliyohifadhiwa katika maghala ya Wakala wa Taifa wa
Hifadhi ya Chakula (NFRA) kanda ya Songea , mkoani Ruvuma alisema
kufuatia taarifa ya kuwepo na baadhi ya maeneo yenye njaa nchini, Serikali imetoa tamko kuwa hakuna mtanzania atayakekufa kwa njaa.
Alisema
serikali kupitia Ofisi ya Waziri Mkuu kitengo cha Maafa imeweka
mikakati ya kukabiliana na tatizo la njaa kwa kutoa msaada wa chakula
katika maeneo yanayokabiliwa na njaa.
“Ni
wajibu wangu kuhakikisha nasimamia vizuri hili, nimeona hali ya
uhifadhi wa chakula, tunayo mahindi ya kutosha lakini hakuna sehemu ya
kuhifadhi chakula” alisema Waziri Mkuu.
Waziri
Mkuu Majaliwa aliendelea kwa kusema uwezo wa maghala hayo yaliyopo
chini ya Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) kanda ya Songea
yana uwezo wa kuhifadhi tani 29 pekee na Songea inauwezo wa kuzalisha
zaidi tani 70 hadi 80.
Pia
, aliagiza Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) kanda ya Songea
, kuanzia mwaka huu kwa kushirikiana na Wakuu wa Mikoa pamoja na Wakuu
wa Wilaya kuanzisha vituo vya kununulia mahindi vijijini na kuhakikisha
magunia yanawafikia wakulima katika vituo hivyo ili
kuwapunguzia mzigo wakulima wa kusafirisha mahindi yao na kuwafanya wayauze kwa bei ya soko.
Alisema wakulima wamekuwa
wakitumia gharama kubwa kuyasafirisha mahindi katika maeneo ya kuyauzia ambapo
wengine wamekuwa wakishindwa na kuwanufaisha mawakala ambao wamekuwa
wakiyauza kwa niaba yao.
Waziri
Mkuu pia, ameitaka Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) kanda
ya Songea ,kutumia teknolojia ya kisasa ya uhifadhi wa chakula, kuandaa
utaratibu maalum utakaozuia msongamano wa malori yanayosubiri kupata
huduma ya kununua mahindi nje ya majengo ya Wakala na kukamilisha miradi
itakayosaidia Wakala kuwa na fedha za kutekeleza majukumu yake.
Kwa
upande wake, Meneja Hifadhi wa Chakula kanda ya Songea, Bwana. Morgan
Mwaipaya alisema kati ya maghala 33 ya kuhifadhi mahindi nchi nzima,
Songea ina maghala 6 kati ya hayo.
Alisema
Wakala imeweka vipaumbele vyake ambavyo ni pamoja na kutoa chakula cha
msaada kwa maeneo yenye matatizo ya njaa, kuongeza upatikanaji wa
mahindi ili kuzuia kupanda kwa bei ya chakula mwaka 2015 – 2016, Wakala
kununua na kuhifadhi mahindi katika maeneo yaliyozalisha zaidi na
kuzingatia sehemu ya sehemu ya akiba ya chakula na kuuza kwa wakulima,
mawakala pamoja na Wakala wa Chakula duniani (World food program).
Alisema
Wakala imeandaa mikakati ya mbalimbali ikiwemo kuongeza uwezo wa tani
24600 hadi tani 45000 kwa mwaka 2014- 2017, kuboresha mfumo wa utendaji
kazi kwa kutumia mifumo ya stahili ya TEHAMA na kutumia fursa za mikopo
kutoka Taasisi mbalimbali za kifedha ili kuendesha shughuli za
uwezeshaji ikiwemo kuelimisha taratibu za ununuzi kwa mawakala.
Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akikagua mahindi yaliyohifadhiwa nje ya majengo
ya maghala ya Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula NFRA mjini Songea
akiwa katika ziara ya siku tatu mkoani Ruvuma Januari 4, 2016.
Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akikagua mahindi yaliyohifadhiwa nje ya majengo
ya maghala ya Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula NFRA mjini Songea
akiwa katika ziara ya siku tatu mkoani Ruvuma Januari 4, 2016.
Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akikagua ujenzi wa Jego la Halmashauri ya Wilaya
ya Peramiho akiwa katika ziara ya mkoa wa Ruvuma Januari 4, 2015.
0 comments:
Post a Comment