Kipute cha Ligi Kuu Uingereza kimeendelea tena leo January 2 kwa michezo kadhaa kuchezwa katika viwanja mbalimbali nchini humo, Man United walikuwa wenyeji wa Swansea City katika dimba la Old Trafford, wakati Arsenal walikuwa wenyeji wa Newcastle United katika dimba la Emirates.
Mchezo ambao ulikuwa na nafasi ya kutazamwa na watu wengi ni mchezo kati ya Man United dhidi ya Swansea City, mvuto wa mchezo huu unakuja kutokana na Louis van Gaal na kikosi chake cha Man United wapo katika wakati mgumu, kiasi cha kuhusishwa kuwa kocha huyo huenda akafutwa kazi.
Man United wakiwa katika dimba lao la nyumbani waliiadhibu klabu ya Swansea City kwa jumla ya goli 2-1, wakati mshambuliaji na nahodha wa Man United Wayne Rooney alipachika goli la pili dakika ya 77 baada ya mshambuliaji wa kifaransa Anthony Martial kupachika goli la kwanza dakika ya 48 na kuanza kumfanya kocha wao Louis van Gaal aanze kutabasamu, Swansea walipata goli la kufutia machozi dakika ya 70 kupitia kwa Gylfi Sigurdsson.
Matokeo ya mechi nyingine za Ligi Kuu soka Uingereza January 2
-
West Ham United 2 – 0 Liverpool
-
Sunderland 3 – 1 Aston Villa
-
West Bromwich Albion 2 – 1 Stoke City
- Norwich City 1 – 0 Southampton
- Leicester City 0 – 0 AFC Bournemouth
- Arsenal 1 – 0 Newcastle United
0 comments:
Post a Comment