Askofu wa jimbo la iringa jonas mkane katika picha . |
Wakristo nchini watakiwa kushirikishana neno la Mungu maana neno ni zaidi ya vitu vyote.
Rai hiyo imetolewa na Askofu wa kanisa la tanzania assemblis of god Jonas Mkane katika ibada ya jumapili ya kwanza ya mwaka mpya 2016,ambapo amesema wakristo wengi wamekuwa ni watu wa kushirikishana mambo ya faida tu kama biashara na mipango mingine ambayo ni ya muda na mwisho wake ni hapa Duniani hivyo amewasihii kushirikishana neno la Mungu ni maaana ni uzima na ni la milele,
Huku aki nukuu kutoka kitabu cha Yeremia 1;17 ambacho kinasema ondoka uende ukawambie niliyokuamuru na kitabu cha Ezekiel 3;17,18, 19.amesema kila muumini ana deni kwa mungu endapo hata fanya kazi ya kuwahubiria watu neno la mungu kwa kuwa damu ya wale watakao kufa dhambini itakuwa juu yao,.
Askofu mkane amesema kanisa linatakiwa kuwa na mpango mkakati wa kumzalia mungu matunda kwa kuwa nia agizo lake kufanya hivyo.
mwisho.BONYEZA HAPA USIKILIZE SEHEMU YA MAHUBIRI YA LEO.
0 comments:
Post a Comment