Watu
wasiojulikana wamevamia na kuvunja ofisi ya kamishna Mkuu wa
Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) na kuiba kompyuta na vifaa
vingine.
Habari
tulizozipata ambazo zimethibitishwa na Polisi kanda maalumu ya Dar
es Salaam zinasema miongoni mwa kompyuta zilizoibiwa ni ile
iliyokuwa inatumiwa na Dr Philip Mpango alipokaimu nafasi ya
Kamishna mkuu wa TRA kabla ya kuteuliwa kuwa Waziri wa Fedha
Kwa
mujibu wa chanzo hicho,huenda kompyuta hiyo ikawa na taarifa muhimu
kuhusu ukwepaji wa kodi na sakata la makontena Bandarini.
Kamanda
wa Polisi Kanda Maalumu Ya Dar es salaam,Simon Sirro amesema tayari
jeshi hilo linawashikilia watu wanne kwa uchunguzi zaidi
Siro alitaja vitu vilivyoibwa katika ofisi hiyo kuwa ni Kompyuta mbili, Televisheni moja na King'amuzi.
Alisema
wanaoshikiliwa ni walinzi wawili kutoka kampuni ya Suma JKT
ambao walikuwa zamu usiku huo, Katibu Muhtasi pamoja na Karani
wa Ofisi hiyo.
0 comments:
Post a Comment