Mapambano ya dawa za kulevya yako kila
kona duniani… najua kukutana na kichwa cha habari kwamba kuna nchi
eti wameamua kuwajengea kabisa vibanda vya kuvutia dawa za kulevya ni
kitu ambacho kinaweza kukushtua, lakini habari iko hivyo !!
Kuna ripoti za watu wenye majina makubwa
duniani kuripotiwa kufariki kwa kuzidisha dawa za kulevya… hizo ripoti
zipo pia zinazowahusu watu wa kawaida ambao ni watumiaji wa dawa hizo… Ireland wameenda mbali kidogo kwa kuamua kuwaokoa watu hao.
Kinachofanyika ni kulegeza kidogo sheria za Ireland,
wako kwenye mpango wa kuanzisha vituo vya kuvutia dawa za kulevya…
kingine ni kwamba kwa sasa mpango wao mwingine ni kuhakikisha
wanaruhusu watumiaji kuwa na kiasi kidogo cha heroin, cocaine na bangi
kwa ajili ya matumizi ya mtumiaji binafsi.
Daktari mmoja amesema kuna wastani wa mtu mmoja kufariki kila siku kwa kujizidishia dawa za kulevya Ireland, lakini duniani kuna maeneo 90 yaliyowekwa maalum kwa watumiaji wa dawa za kulevya na haijawahi kutokea mtu akafariki.
Kwenye utetezi wa uamuzi wao, Ireland
wamesema kwenye vibanda hivyo kutakuwa na usimamizi mzuri utakaofanya
wanaojidunga wasizidishe kiwango cha dozi ya dawa na kutokea matatizo
mengine.
0 comments:
Post a Comment