KWA TAARIFA YAKO - LICHA YA KUPATA MCHUMBA MALOPE HATAKI NDOA, PIA AFADHILIWA KWA KUPIGWA MAKOFI NA WAIMBAJI WAKE
Haya msomaji wetu wa Gospel Kitaa karibu katika kipengele chetu cha ''KWA TAARIFA YAKO''
ambacho kinakujia kila siku za alhamisi ndani ya GK kikiwa na lengo la
kukupatia habari ambayo iliwahi kutukia lakini yawezekana huijui pia
yawezekana ilitukia ukawa unaijua lakini GK ikawa imesahau mahali au
kuna sehemu haina usahihi utapata fursa ya kusahihisha kwa kuweka
comment yako chini kabisa kwenye habari husika. Karibu
Rebecca akiwa na mchumba wake bwana Tshabalala walipokuwa kwenye mahojiano WAPO Radio FM. |
Leo katika kipengele cha KWA TAARIFA YAKO tunaelekea huko nchini Afrika ya kusini ambako tunakutana na mwanamama malikia wa muziki wa gospel barani Afrika bibie Rebecca Malope
mama huyu ambaye ana umri wa miaka 44 sasa ni kwamba kama tulivyowahi
kuandika alipotembelea nchini mapema mwaka huu wakati wa pasaka kwamba
baada ya kukaa mpweke kwa miaka mingi mwanamama huyu kwasasa amepata
mchumba aitwaye Themba Tshabalala.
Mchumba ambaye pia alikuja naye nchini, lakini linapokuja suala la
kufunga ndoa mwanamama huyu anasema bado mapema saaana kwani anataka
kwanza wafahamiane vyema na mchumba wake huyo ambaye pia ni mmoja wa
mameneja wake. Amesema mpaka sasa amewakataa wanaume watatu waliokuwa
tayari kumuoa kwasababu hakuwa tayari, ila anadhani mwanaume huyu ndio
mwafaka ingawa anasema bado yupo yupo kwanza kwenye suala la kufunga
ndoa.
VITUKO VYA WAIMBAJI ALIOWATOA KIMUZIKI
Mwanamama huyu ambaye anamafanikio sana kwenye medani ya muziki barani
Afrika, amewatoa waimbaji wengi sana akiwemo Lundi Tyamara mwanakaka
ambaye ukisikiliza sauti yake inafanana na Rebecca, pia ni mwimbaji
aliyekuwa mwitikiaji katika band ya Malope, lakini cha ajabu ni kwamba
kati ya waimbaji wawili waliokuwa wanataka uadui na Rebecca ni mwanakaka
huyu na dada mwingine ambaye alidiriki hata kumpiga makofi Rebecca
kutokana na kile kwamba mwimbaji huyu anakubalika sana, kufuatia tukio
hilo Rebecca alikaa kimya ingawa vyombo vya habari nchini humo
viliandika tukio hilo.
Pamoja na hayo Rebecca ameendelea kusimama katika huduma pamoja na
mashambulizi na maneno mengi yaliyowahi kusemwa juu yake na waimbaji hao
likiwemo suala la mwanamama huyo kuhusishwa na ulevi wa pombe,
kilichofanyika kwa sasa waimbaji hao wamejirudi na kumuomba msamaha
mwanamama huyo huku Lundi akiwa tayari amejishusha kabisa katika suala
la Gospel kutokana na shutuma nyingi juu yake kutoka katika vyombo vya
habari.
0 comments:
Post a Comment