|
Yvonne Chakachaka katika pozi. |
Kundi la Soweto Gospel Choir (S.G.C) jumatatu iliyopita lilikuwa studio
pamoja na kundi la Black Mambazo wakirekodi video ya wimbo ''A
Magnificent Man'' walioshirikishwa na mwanamama Yvonne Chakachaka ukiwa
maalumu kwa ajili ya heshima ya Rais wa kwanza wa nchini kwao Nelson
Mandela ambaye mwezi huu atakuwa akitimiza miaka 94 tangu kuzaliwa
kwake.
Kwa mujibu wa taarifa zilizotolewa na kundi la Soweto Gospel Choir
ambalo pia ni balozi katika mfuko wa Rais huyo mstaafu wamesema, wimbo
huo utaonyeshwa tarehe 18 mwezi huu umoja wa mataifa(UN) ikiwa siku ya
kuadhimisha kuzaliwa kwa mzee Madiba. Waimbaji binafsi na makundi
mbalimbali nchini Afrika ya kusini yamekuwa katika matayarisho
mbalimbali kwa ajili ya kusherehekea sikukuu ya kuzaliwa kwa rais wao
huyo wa kwanza kuchaguliwa kidemokrasia tangu ulipoisha utawala wa
makaburu nchini humo.
|
Kundi zima la Soweto Gospel Choir katika picha ya pamoja. |
|
Baadhi ya waimbaji wa S.G.C nyuma ya jukwaa. |
0 comments:
Post a Comment