Home » »

MAKALA : SIZE 8 ALIKOSA AMANI MOYONI KUIMBA NYIMBO ZA KIDUNIA



Tarehe 12 April mwaka huu ilikuwa siku ya kipekee sana kwa wapenzi wa muziki wa gospel na wale ambao wameokoka baada ya mwimbaji maarufu aliyekuwa akitengeneza pesa nyingi na kupendwa na mashabiki wa muziki wa nje ya kanisa kuamua kumrudia Mungu wake na kutangaza kuachana na muziki huo aliokuwa akiufanya awali na kurudi kanisani.

Huyu si mwingine bali mwanadada Linet Munyeli ama mwite size 8 jina lake maarufu huyu ni mwimbaji wa gospel kutoka pale nchini Kenya, mwimbaji huyu aliyetamba na nyimbo mbalimbali nchini humo hasa wimbo unaojulikana uitwao vidonge.

Mapema mwaka huu aliamua kumpa Yesu maisha yake baada ya kuishi maisha yakutokuwa na furaha na amani kwa muda mrefu licha ya kuwa na vitu ambavyo watu hudhani ukiwa navyo umewezea maisha. Linet alikaririwa akisema kwamba licha ya kwamba alikuwa akipata fedha nyingi na kuwa na mashabiki wengi sana lakini moyo wake haukuwa na amani hata kidogo jambao ambalo lilikuwa likimuhuzunisha hivyo kuamua kumrudia muumba wake.




Linet ambaye ni mtoto wa sita katika familia yao ambayo wazazi wake wote ni wahubiri na kwamba katika muda wote aliokuwa akiimba mziki wa dunia mama yake alikuwa akimuombea kila siku ili abadilike na kumwimbia Mungu wake jambo ambalo liliwezekana na Mungu kumuokoa binti huyo mapema mwaka huu. Linet alisimama kwa muda kuimba muziki wa dunia kumbe wakati huo alikuwa anarekodi wimbo ambao unatamba kwasasa uitwao "Mateke" ambapo wakati wote wa kurekodi amesema alifanya siri kubwa ili watu wasijue ili ije kuwa kama kuwastukiza watu ambapo amesema alirekodi wimbo huo "Mateke" chini ya Jack B wa Tamu sana records kisha video yake akarekodi na Princecam media.

Kwa wakati wote huo aliweza kutunza siri hiyo ambayo haikuvuja mpaka pale wakati alioutaka yeye kuwaambia Wakenya na watu wengine kwamba yeye ameokoka, siku hiyo ndiyo ilikuwa tarehe 12 April 2013 siku ambayo ilitangazwa na DJ Mo wa NTV kwamba mwimbaji huyo ameachana na muziki wa kidunia kwasasa anaimba muziki wa injili akiwa na ushahidi pia wa wimbo huo wa "Mateke" ambao umemtambulisha vyema kwenye uimbaji wa kumsifu Mungu.
Facebook Blogger Plugin: Bloggerized by Joseph Kipangula Enhanced by Joseph Kipangula

0 comments:

Post a Comment

NURU FM 93.5 IRINGA

.

.

.

Nyali

Pages

Pages

Powered by Blogger.

Blog Archive

Search This Blog