MAAJABU:- KIJANA AFUMANIWA AKIMBAKA NG'OMBE WA JIRANI YAKE ZIZINI - MBEYA
Katika
hali isiyokuwa ya kawaida mtu mmoja aliyejulikana kwa jina la Tumsifu
Mwambusi (20),mkazi na mkulima wa Kijiji cha Mwela,Wilaya ya Rungwe
Mkoani Mbeya amefumaniwa akimbaka ng’ombe.
Tukio
hilo la ajabu yake limetokea Julai 15 mwaka huu majira ya saa mbili za
usiku ambapo jamaa huyo alikwenda kwenye makazi ya Bwana Leonard
Mwangwemba,kisha kuingia ndani ya zizi na kuanza kumbaka ng’ombe huyo
hali iliyopelekea ng’ombe huyo kuanza kupiga kelele kwa kuomba msaada.
Ndipo
wakazi wa eneo hilo walielekea eneo la tukio na kumkuta kijana huyo
akiendelea na kitendo hicho na kumshushia kipigo cha mbwa mwizi mara
baada ya kuvunja amri ya sita ya kuzini na ng’ombe huyo.
Aidha,kufuatia
hali hiyo Kijana Mwambusi aliomba msamaha kwa kitendo hicho lakini
wananchi hao hawakujali na mara akajikuta akimwagiwa maji ya baridi na
kipigo kikiwa kinaendelea na kusababishiwa maumivu sehemu mbalimbali ya
mwili wake.
Hata
hivyo wazazi wa kijana huyo walijaribu kutoa kiasi cha shilingi 100,000
kwa wananchi hao ili waweze kumwachia kijana wao kufuatia kipigo
alichokuwa akipewa.
Kwa
upande wake mwenyekiti wa kijiji hicho Bwana Andongwisye Mwakalinga
amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na amewasihi wananchi hususani
vijana kumwomba mungu muda wote ili kuondokana na majaribu
yasiyompendeza Mwenyezi Mungu.
0 comments:
Post a Comment