Kekeletso maana yake Maongezeko
* Baada ya Tour yake na Dube ilimtoa kwa kiasi kikubwa kwa kumfanya ajulikane na kujiunga na Joyous Celebration
* Uwezo
wake wa kuimba, kulimiliki jukwaa, pamoja na Kuhubiri kwa Nguvu kubwa
za Roho mtakatifu ndivyo vitu vinavyomtofautisha sana Keke na
Mwanamuziki yeyote umjuaye wa nyimbo za Injili Duniani.
Kekeletso Phoofolo ama “KEKE” kama ajulikanavyo kwa wengi Barani afrika na Duniani kote ni Mwanamuziki wa Muziki wa Injili kutoka nchini A frika ya Kusini. Kekeletso maana yake Maongezeko, Keke alizaliwa katika kitongoji cha Pimville kilichoko Mjini Soweto nchini Afrika ya Kusini. Kadri alivyokuwa akikuwa ndoto yake kubwa ilikuwa ni kujiunga na Jeshi la nchi hiyo.Ndoto yake hiyo haikuweza kutimia kwa kuwa pamoja alikuwa akipenda jeshi pia alikuwa akipenda sana muziki.
Mwaka
1994 Keke alianza rasmi kujishughulisha na Muziki ambapo alijiunga na
kundi la Zoe Gospel Music akiwa kama Back Vocalist. Mwaka 1997 Keke
alikuwa na uwezo wa kufanya kazi zake binafsi akiwa kama Solo artist.
Wakati akifanya kazi zake binafsi mnamo mwaka 1998 alipata tena nafasi
ya kujiunga na kundi lingine la Muziki wa injili nchini humo
lijulikanalo kama Kom Kom. Mwaka 1999 Keke alipata nafasi ya kufanya
Tour na Nguli wa Muziki wa injili nchini humo Benjamini Dube.
KEKE ON THE STAGE |
Baada
ya Tour na Dube ambayo ilimtoa kwa kiasi kikubwa kwa kumfanya
ajulikane, Keke alijiunga na Joyous Celebration mwaka 2000-2001 akiwa
miongoni mwa ma –solorist wa Kundi hilo linaloaminika kuwa is the most
leading Gospel Group in Afrika. Akiwa na Joyous, Keke ali-lead kwenye
nyimbo iitwayo ‘Jo Ke Mohlolo-Hlolo’
(Joyous 6) kabla hajaondoka kundini humo. Baada ya kutoka Joyous Keke
alifanya Kazi na wanamuziki wengi akiwemo Bheki Mseleku, Winston
Mankunku na kundi la Umoja Choir.
Malkia
wa Swazlland alimuomba Keke atengeneze Live Recording Project chini ya
Redemption Choir kitendo ambacho kilimpa keke nafasi ya kufanya kazi
katika nchi jirani na Afrika ya Kusini hiyo ikiwa ni mwaka 2001-2004.
Mwaka 2006 keke aliamua kuanza kufanya kazi zake binafsi. Album yake ya
kwanza iliitwa “REVIVAL” ambayo ni LIVE DvD ilirekodiwa katika Chuo
kikuu cha Ufundi cha Vaal cha nchini humo. Wakati akizindua album hiyo
Keke alisema “Wakati umefika sasa kwa waafrika kuondokana na dhana ya
kuwa Omba omba kwa kuwa tuna nafasi ya kupata kile tunacho kihitaji”
MAFANIKIO
Keke akichukua moja ya Awards
Tofauti na Kuimba, Keke ni ni Mtumishi wa Mungu anayesimama katika Ofisi ya Kinabii, Prophet Keke anaongoza kanisa liitwalo SHERKINAH GLORY WORSHIP TABERNACLE. Keke ni Baba wa watoto watatu na anaishi na kuhudumu na Mkewe. Uwezo wake wa kuimba, kulimiliki jukwaa kwa namna ya pekee, pamoja na Kuhubiri kwa Nguvu kubwa za Roho mtakatifu ndivyo vitu vinavyomtofautisha sana Keke na Superstar yeyote umjuaye wa nyimbo za Injili Duniani.
0 comments:
Post a Comment