Wakati hapo Leo ndio kilele cha
utolewaji wa tuzo za Africa Gospel Music Awards 2012 mmoja kati ya
waimbaji waliokuwa wakitazamiwa kuimba katika sherehe hizo
zitakazofanyika jijini London nchini Uingereza ametangaza kutokuhudhuria
katika sherehe hizo.
Mwimbaji huyo kutoka katika kundi la Joyous Celebration kijana Mkhululi
Bhebhe ambaye alianza kutangazwa kushiriki toka hatua za awali za
maandalizi ya tuzo hizo, amefunguka kupitia ukurasa wake wa Facebook na
kusema kwamba kutoshiriki kwake kunatokana na sababu zisizoweka
kuzuilika. Ukiacha Mkhululi waimbaji wengine wanaotarajiwa kuwepo hiyo
kesho ni pamoja na kundi la Makoma, Sonnie Badu, Ephraim Sekeleti na
waimbaji wengine kutoka Afrika Magharibi.
Home »
» MWIMBAJI WA JOYOUS ATANGAZA KUTOSHIRIKI UTOLEWAJI WA TUZO ZA AFRICA GOSPEL HII LEO
MWIMBAJI WA JOYOUS ATANGAZA KUTOSHIRIKI UTOLEWAJI WA TUZO ZA AFRICA GOSPEL HII LEO
Posted by Unknown
Posted on 8:10 PM
with No comments
Facebook Blogger Plugin: Bloggerized by Joseph Kipangula Enhanced by Joseph Kipangula
0 comments:
Post a Comment