Kundi la Ambassadors of Christ Choir kutoka kanisa la wasabato Remera
jijini Kigali nchini Rwanda, linategemea kuingia nchini Kenya kwa mara
nyingine mwaka huu ikiwa ni mwaliko wa kwenda kushiriki kambi za
kikristo zinazoandaliwa na kanisa hilo katika nchi mbalimbali.
Kwa mujibu wa taarifa ambazo GK imezipata ni kwamba kwaya hiyo itakuwa
nchini Kenya kuanzia July 26 hadi 30 mwaka huu huko Migori eneo la
Awendo. Itakuwa mara ya pili kwa kwaya kwa mwaka huu kufanya huduma
nchini Kenya ambapo walikuwa huko mapema mwezi wa tano, kwasasa kwaya
hiyo inatamba na album mpya waliyoitoa mapema mwezi uliopita
walipotembelea nchini.
 |
Baadhi ya waimbaji wa Ambassadors of Christ wakimsifu Mungu. |
 |
Baadhi ya wakaka wa Ambassadors of Christ wakishambulia jukwaa walipotembelea jijini Dar es salaam. |
 |
Warren
katikati na waimbaji wenzake wa Ambassadors of Christ Rwanda,
Warren(mtanzania) amekuwa mmoja wa waimbaji wa kundi hilo kutokana na
ukaribu wake na waimbaji wa kundi hilo la Rwanda.picha kwa hisani ya
Warren |
0 comments:
Post a Comment