HIVI NDIVYO MWANANCHI WA KIJIJI CHA WENDA ALIVYOCHUNWA NGOZI
Hivi ndivyo mkazi wa Wenda alivyochunwa ngozi na watu wasiojulikana (Tunaomba Radhi kwa picha hizi )
Hii ndio nyumba ulimokutwa mwili wa mkazi huyo
eneo la tukio
Baada ya siku mbili mtandao huu kuripoti
tukio la kusikitisha kilichohusisha mauaji ya kinyama ya dereva wa
bodaboda sadiki mbelwa (26) katika kijiji cha wenda, Tanangozi Iringa
ambapo mwili wa marehemu ulikutwa ukiwa na majeraha sehemu za kichwani
huku ikisadikiwa kupigwa na kitu chenye ncha kali.
eo katika tukio lingine la kusikitisha
ambalo limetokea katika kijiji cha wenda kitongoji cha Lupeta amekutwa
mwili mwanakijiji aliyetambulika kwa jina la Leornad Kutika (49.
Mwili wa marehemu kutika umekutwa katika
nyumba aliyokuwa akiishi huku ukiwa umechunwa ngozi, kunyofolewa macho
pamoja na kukatwa sehemu za siri.
Akingea na mtandao huu wa huzuni baba
mdogo wa marehemu Martin Kutika mkazi wa lupeta anaeleza kuwa usiku wa
kuamkia jana alipigiwa simu ndugu wa marehemu aliyefahamika kwa jina
Kibadeni kutika kuwa ndugu yake huyo ambayekwa mujibu wa maeezo yake
alikuwa akisumbuliwa na tatizo la akili alikutwa katika nyumba aliyokuwa
anaishi huku akiwa amefariki na kuondolewa sehemu za siri na kuchunwa
ngozi. Zwadi mwenga ambaye pia ni ndugu wa marehemu anaeleza kuwa
alipata taarifa za tukio hilo jana na ndipo alipofika katika nyumba ya
marehemu na kukuta akiwa amefariki.
Akilelezea kuhusu tatizo alilokuwa nalo
marehemu Mwenga amesema marehemu alianza kusumbuliwa na tatizo la
kurukwa akili tangu alipokuwa mdogo japo hakuwahi kufanya vurugu yoyote
na wao kama familia wamekuwa wakimpatia chakula na siku mbili kabla ya
tukio marehemu alionekana lakini baada ya hapo hawakumuona tenda ndipo
wifi yake alipofika nakukuta marehemu amekufa huku akiwa ametendewa
unyama huo.
Afisa mtendaji wa kijiji cha wenda
Dismas Ngweta anaeleza kuwa alipigiwa simu na mwenyekiti wa kjjij cha
lupeta Geofrey Dugange nakumweleza kuwa hakuna amani katika kijiji hicho
kuwa kuna mwanankijiji ambaye ameuawa. Akielezea baada ya kufika eneo
la tukio Ngweta anaeleza kuwa walipouangalia mwili wa marehemu
waligundua kuwa amechunwa ngozi, kunyofolewa macho, kukatwa sehemu za
siri pamoja na kutobolewa katika sehemu ya mguu. Akilinganisha tukio
hili na lililotokea siku chache zilizopita Ngweta ameeleza kuwa tukio la
dereva wa bodaboda limetokea wakati wa usiku na kusema kuwa inasemekana
kuwa tukio la pili limetendeka usiku kwani kwa mujibu wa wanakiji
walieleza kumwona marehemu jioni kabla ya tukio.
Je nijuhudi gani zimefanywa na jeshi la
polisi mpaka sasa? Ngweta ameeleza kuwa baada ya kupata taarifa ya
tukio hilo alipiga simu kwa mkuu wa kituo cha ifunda naye akajibu kuwa
awasiliana na wa kituo kikubwa Iringa. Mpaka mtandao huu unatoka eneo la
tukio hakuna afisa usalama aliyekuwa amefika katika eneo hilo.
Tukio hili ni la mara ya pili kutokea
baada ya tarehe 25 Septemba kuripotiwa kuuwawa kinyama kwa dereva wa
bodaboda na pikipiki yake kutoonekana.
0 comments:
Post a Comment