KAMPUNI ya Simba Logistic Equipment Supply yazindua kifaa cha kuzimia moto kwa kurusha kiitwacho B
KAMPUNI
ya Simba Logistic Equipment Supply hivi karibuni ilizindua kifaa cha
kuzimia moto kwa kurusha kiitwacho Bonex ambacho vinatumia kuzimia moto
katika majumba, magari na sehemu nyinginezo.
Akizungumza
na waandishi wa habari wakati wa hafla ya uzinduzi wa vifaa hivyo
Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Simba Logistic Equipment Supply Co
Limited, Fareed Nahdi alisema kuwa vifaa hivyo ni rahisi kutumika katika
matukio mbalimbali ya kuzimia moto.
Alisema kuwa havihitaji matengezo ya mara kwa mara kwa kuwa vikinunuliwa vinatumika kwa mara moja kwa tukio moja.
Alisema
kuwa ni vifaa ambavyo ni rahisi kubebeka na kutumika katika mazingira
yoyote kutokana na udogo wake ambao unaumuhimu mkubwa katika kuzima
moto.
“Hii
ni aina mpya ya uzimaji moto kwa kutumia vifaa hivi muhimu ambapo
ukitofautisha na vifaa vingine ambapo kunakuwa kuna maelekezo mengi ya
kufuata lakini hiki unarusha tu hivyo hata watoto wanaweza
kutumia”alisema Nahdi.
Alisema kuwa hakina madhara kama vile moshi wala aina nyingineyo ya madhara na kinasaidia harakati za uokozi wa wat.
Naye
Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani Mohamed Mpinga aliyekuwepo
kushuhudia uzinduzi huo alisema kuwa kifaa hicho kinaweza kusaidia zaidi
hata katika kuzima motoo wa magari.
Alisema kuwa wenye magari wanapaswa kwua na kifa hicho kwa kuwa ni rahisi kutumika pia.
0 comments:
Post a Comment