900 waliuawa katika vita dhidi ya M23
Jeshi la congo linasema kuwa mapigano na waasi wa M23 yamesababisha vifo vya zaidi ya wapiganaji 900 tangu mwezi Mei.
Msemaji wa jeshi Genarali Jean-lucien
Bahuma alisema kuwa takriban wanajeshi 200 na zaidi ya wapiganaji 700
waliuawa katika mapigano katika eneo la Mashariki mwa Jamhuri ya
Kidemokrasia ya Congo.Wanajeshi watatu wa amani wa UN pia waliuawa
kwenye makabiliano hayo.
Pia wapiganaji 72 wa Rwanda na wapiganaji 28 wa Uganda waliuawa.
Mwanzoni mwa mwezi huu, waasi wa M23 walitolewa na jeshi la serikali
iliyoungwa mkono na kikosi cha wanajeshi wapatao 5000 wa Umoja wa
Mataifa lakini serikali ya Congo na waasi walikosa kuelewana kuhusu
mpango wa baadae wa amani.
Waasi wa M23 walisitisha vita na kujisalimisha baada ya jeshi la DRC kwa
ushirikiano na wanajeshi wa UN kupigwa vita vikali na kuwaondosha
katika maeneo waliyokuwa wameyateka.
Maelfu ya wakaazi wa Mashariki mwa DRC walilazimia kukimbilia nchi
jirani ya Uganda kutafuta hifadhi wakati kundi hilo lilipokuwa
linaendesha uasi wao na hata kuuteka mji wa Goma kwa muda.
Kudni la M23 lilifanya vitendo vya kikatili dhidi ya watu wa Mashariki
mwa DRC ikiwemo ubakaji na kuwatumia watoto kama wapiganaji.
0 comments:
Post a Comment