YAYA TOURE AITISHIA AMANI CHELSEA, AWAAMBIA REKODI YAO IKO HATARINI
KIUNGO Yaya Toure anaamini Manchester City inaweza kuvunja rekodi ya mabao ya msimu katika Ligi Kuu England msimu huu.
Kiungo
huyo wa nguvu amempa jeuri kocha Manuel Pellegrini juu ya uwezo wa
kushambulia unaoleta matumaini ya taji kwa kusema rekodi ya Chelsea iko
hatarini.
Kocha
Carlo Ancelotti akiwa na kikosi mariadi msimu huu 2009-10 aliiwezesha
Chelsea kufunga mabao 103 na kutwaa taji misimu minne iliyopita.
Jitu la nguvu: Yaya Toure (kushoto, akipambana na Paulinho wa Spurs, amesema City inaweza kuvunja rekodi ya mabao
Mabao sita: Sergio Aguero alifunga mabao mawili City ikiifumua Tottenham Jumapili
Inua mikono juu: Chelsea ilifunga mabao 103 wakitwaa ubingwa wa Ligi Kuu mwaka 2010
Na baada ya timu ya Pellegrini kufikisha mabao 34 wakiifunga sita Spurs Jumapili, Toure amesema lengo ni kuvunja rekodi hiyo.
Alipoulizwa kwamba inaezekana kuipiku rekodi ya Chelsea, alijibu: "Natumaini hivyo — tuna washambuliaji. Watu wawili mbele (Alvaro Negredo na Sergio Aguero) hawa watu huwezi kuamini. Wanajiamini sana.
"Lakini
si kwa sababu ya wachezaji hao wawili tu. Ni timu nzima. Tunashambulia
sana na washambuliaji wote wanafurahia hii. Hata (Edin) Dzeko na
(Stevan) Jovetic.
"Timu
inaelekeza nguvu zake katika kushambulia. Ni babu kubwa. Na unaposhinda
kama tulivyofanya kwa Tottenham ni nzuri. Ni washindani wa kweli katika
mbio za taji la Ligi Kuu mwaka huu,".
Nje ya Uwanja: Lakini hata Edin Dzeko anafurahia maisha namna ambavyo City inafunga mabao, amesema Toure
0 comments:
Post a Comment