Home » »

BABA WA GWIJI LA MUZIKI WA GOSPEL DUNIANI AFARIKI DUNIA

Donnie McClurkin.
Baba mzazi wa gwiji la muziki wa injili duniani Donnie McClurkin's aitwaye Donald Andy McClurkin amefariki dunia hapo jana majira ya saa 10 alfajiri kwasaa za Marekani. Mzee huyo amefariki dunia ikiwa ni wiki moja tangu alazwe kutokana na kufanyiwa upasuaji wa dharura katika hospitali ya Palmetta Baptist Medical iliyoko kaskazini mwa mji wa Carolina.

Kupitia katika ukurasa wake wa Facebook Donnie aliandika ujumbe huu "
Donnie Mac my greatest loss this year is that of my parents…this man…my hero has left and gone away…gone home~!"

Taarifa zaidi juu ya mazishi na taratibu za msiba huo bado hazijatolewa na familia, waimbaji, wapenzi na mashabiki wa muziki wa gospel wa gwiji huo wamepokea kwa masikitiko taarifa za msiba huo, ambapo kwa nyakati tofauti wamekuwa wakimtumia meseji za faraja Donnie na familia yake kutokana na msiba huo. Mmoja kati ya waimbaji hao ni Yolanda Adams ambaye ameandika kupitia ukurasa wake wa Facebook na tovuti yake juu ya msiba huo.

Dannie ambaye mama yake mzazi alishafariki dunia, awali amewahi kuwa na matatizo na baba yake hali iliyofanya kutokuwa na mawasiliano naye, lakini Mungu akafanya njia kwa mwimbaji huyo kutengeneza na baba yake na kuamua kumchukua kuishi naye nyumbani kwake, ambapo miaka ya karibuni mwimbaji huyo aliwahi kueleza kwamba anaishi vizuri sana na baba yake  wamekuwa marafiki wakubwa na kwamba haitakuja kutokea kumtolea sauti ya ukali baba yake ama kumkwaza.


ANGALIA VIDEO HII DONNIE AKIONYESHA HISIA ZAKE NA FURAHA YAKE YA KUWA NA BABA YAKE KARIBU, WAKATI AKIHOJIWA NA   BISHOP TD JAKES,

Facebook Blogger Plugin: Bloggerized by Joseph Kipangula Enhanced by Joseph Kipangula

0 comments:

Post a Comment

NURU FM 93.5 IRINGA

.

.

.

Nyali

Pages

Pages

Powered by Blogger.

Blog Archive

Search This Blog