BALOTELLI AZUA LINGINE ITALI BAADA YA KUTWEET "THIS IS THE END"
MSHAMBULIAJI
Mario Balotelli amewachangasha tena mashabiki wake leo baada ya kutweet
'this is the end' (huu ni mwisho) saa kadhaa baada ya kukosa penalti AC
Milan ikilazimishwa sare ya 1-1 na Genoa.
Mshambuliaji
huyo hatari, alitweet ujumbe huo Kiingerezamajira ya saa 11 Alfajiri
kwa sa za kwao katika akaunti yake ya @finallymario.
Pamoja
na hayo, saa sita baadaye akatuma ujumbe mwingine wa tweet Kitaliano,
uliosomeka: ‘Forza Milan comunque e sempre.’ ambao Kiingereza ni 'Go on
Milan, no matter how and forever'.
Mwisho wa barabara? Mario Balotelli alikosa penalti timu yake AC Milan inayosuasua ikilazimishwa sare ya 1-1 na Genoa
Anamaanisha nini? Balotelli ametweet baada ya sare ya AC Milan na Genoa
Balotelli akipiga penalti aliyokosa
Hakuna furaha: Balotelli amekosa penalti mbili msimu huu
0 comments:
Post a Comment