BINTI ATISHIWA KUCHINJWA NA KUSILIMISHWA KWA NGUVU NIGERIA
Hajja ©Reuters/Joe Brock |
"Nilipolia walinipiga, na nilijaribu kuongea pia walinipiga. Waliniambi
aninlazima nisilimu kuwa Muislamu ili wasiniue". Hajja anasimulia, binti
mwenye umri wa miaka 19, ambaye amepona kwenye mikono ya kundi la
kigaidi lenye uhusiano na al-Qaeda, Boko Haram nchini Nigeria.
Milima ya Gwoza ndiko ambako kijiji cha binti Hajja kinapatikana, ambapo
kuna siku alikuwa kwenye shughuli za kawaida alipotekwa na kundi hilo,
na kulazimishwa kuzunguka nalo kwa miezi mitatu huku akiwapikia na
kuwafulia nguo zao.
Katika ushuhuda ambao ameueleza kwa shirika la habari la Reuters, Hajjaa
anasema kuwa. licha ya kwamba hakubakwa, ila alikuwa akiteswa vibaya
sana na kulazimishwa kuachana na Ukristo, ili apate kuishi, jambo ambalo
alikuwa akipingana nao kwa nguvu, hatua ambayo ilimfanya mmojawapo wa
watekaji kumbembeleza ili asiuawe kwa kuchinjwa, ambapo siku moja kabla
tu hajauwawa ilimbidi akubaliane nao na kuapishwa - na kisha
kulazimishwa kusoma Quran.
Kati ya mayeso ambayo ameyapata, Hajja anaeleza kuwa alikuwa ni mtu wa
kufua na kupika, na kama hakuwa akifanya hizo shughuli basi
alilazimishwa kubeba silaha zao, na kisha siku moja hatosahau ni pale
ambapo walimfanya chambo/mateka mbele ya wanajeshi wa serikali ili
wasidhurike wala kukamatwa.
0 comments:
Post a Comment