HAYAWI HAYAWI HATIMAYE YANAKUA, NI JUMAPILI HII
Uzinduzi huo unaotarajia kusindikizwa na waimbaji kama Miriam Lukindo,
The next level team, Upendo Nkone, Florence Mureith kutoka Kenya, Rivers
of Joy, Zion band pamoja na kundi la Acapela The Voice, kiingilio
katika uzinduzi huo ni shilingi 10,000. Kundi la GWT ambalo limesheheni
vijana wenye vipaji mbalimbali katika tasnia ya kumtukuza Mungu hadi
kufikia bendi zinazopiga miziki ya kidunia kuwashawishi baadhi ya
waimbaji na wapigaji wa kundi hilo kujiunga nao wamekuwa wakigonga
mwamba kutokana na msimamo thabiti wa vijana hao katika kumtumikia
Mungu.
Kwasasa kundi hilo limekamilika kila idara, uimbaji, upigaji, maombi
pamoja na uongozi wake madhubuti kutoka kwa kijana Emanuel Mabisa ambaye
alianza kuliongoza jahazi la kundi hilo tangu hawajatoka katika kundi
la Glorious Celebration ambako ndiko walitoa album ya kwanza iitwayo
Niguse.
Wapigaji wa GWT wakijifua tayari kwa kumtukuza Mungu jumapili. |
0 comments:
Post a Comment