Hivyo
aliwataka wahitimu wa
chuo hicho kuendelea
kutoa ushirikiano kwa chuo hicho na
pale michango yao inapohitajika kwa ajili ya kuendeleza
ujenzi wa majengo ya
chuo hicho kutoa ushirikiano wao.
Huku makamu
mkuu wa chuo hicho
Prof Joshua Mwadumulla alisema wakati chuo
hicho kinasherekea mahafali haya ya 18 toka
kuanzishwa kwake bado wanatambue kuwa kumekua na ushindani
mkubwa katika uga wa elimu ya juu kutokana na kuweko kwa ongezeko kubwa la vyuo
vikuu katika Tanzania
“….Mwanzoni mwa miaka ya 70,kulikua na chuo
kikuu cha Dar es salaam peke yake kikiwa na matawi mawili ambayo ni muhimbili
na sokoine….leo hii baada ya miaka 40 tunazungumzia idadi inayokaribia 60 ya
vyuo vikuu katika Tanzania….lakini idadi ya wanafunzi inayotakiwa kudahiliwa na
vyup hivyo haijaongezekea sana….ndiyo maana kumekua na uhaba wa udahili wa
wanafunzi….Uhaba huo umesababisha ushindani kubwa wa mahitaji ya wanafunzi…ndiyo
maana kuna haja ya chuo kikuu cha Iringa kuwa na mikakati mizuri ya kuongeza udahili kwa
wanafunzi”
Akizungumzia mikakati hiyo Prof Mwadumulla alisema kuwa wanajitahidi
kuanzisha program ambazo zina upekee Fulani
ili kuweza kuanza kuachana na mfumo wa kijadi ya kuigana katika biashara Fulani
ambazo mtu humuona mtu mwingine akifanikiwa kupitia biashara hiyo kutokana na
biashara ya namna hiyo kuwa na faida kwa mazoea na kufahamiana na si kwa upekee
na ubora.
Program nyingine zilizoanzishwa na chuo hiko
ili kupambana na tatizo la ajira nchini Prof.Mwadumulla alisema kuwa wana program
inayoitwa Team Academy yaani academia shirikishi inayomtaka mwanafunzi asome
kwa vitendo zaidi tena kwa ubunifu kupitia nadharia ya darasani kuliko kuwa
kasuku wa uradidi wa nadharia.
0 comments:
Post a Comment