Home » » TAHADHARI YA MATAPELI MKOANI IRINGA PLZ MSIKILIZE KAMANDA HAPA CHINI USIJE UKALIZWAA

TAHADHARI YA MATAPELI MKOANI IRINGA PLZ MSIKILIZE KAMANDA HAPA CHINI USIJE UKALIZWAA


Jeshi la polisi mkoani Iringa limetoa tahadhari kwa wananchi juu ya matapeli wawili wanaume ambao wanadaiwa kuwateka wananchi kwa kuwapa dawa na kisha kutapeli mali zao. Akitoa tahadhari hiyo kamanda wa polisi mkoa wa Iringa ACP RAMADHAN MUNGI ameelezea wasifu wa watu hao kuwa ni mmoja mrefu mweupe na amechora tattoo mikononi na mwingine ni mfupi mweusi. SAUTI ACP 1 Aidha kamanda Mungi amesema kuwa watu hao waliweza kumteka binti mmoja kwa kumlaghai kuwa wanaweza kumtatulia matatizo yake na kumpa dawa iliyompumbaza akili kisha kumpeleka katika kichaka eneo la frelimo manispaa ya Iringa na kumbaka. SAUTI ACP 2 Kamanda Mungi amewasihi wananchi kutoa taarifa za watu wanaowatilia mashaka na kuongeza kuwa Jeshi la polisi linaendelea na msako ili kuweza kuwatia mbaroni wahalifu hao.
Facebook Blogger Plugin: Bloggerized by Joseph Kipangula Enhanced by Joseph Kipangula

0 comments:

Post a Comment

NURU FM 93.5 IRINGA

.

.

.

Nyali

Pages

Pages

Powered by Blogger.

Blog Archive

Search This Blog