Rais John Magufuli amelaani vikali kitendo cha Wabunge wa Vyama vya Upinzani kuzomea leo bungeni.
Rais
Magufuli ameeleza kuwa tabia iliyofanywa na wabunge hao inaonesha jinsi
ambavyo hawajakomaa kisiasa na kuwaita watoto huku akimpongeza Mbunge
wa Kigoma Mjini, Zitto Kabwe kwa kuendelea kubaki Bungeni.
“Ndio maana nimempongeza sana Mheshimiwa Zitto. Mheshimiwa zitto umekomaa na naamini hata wana CCM kule Kigoma walikuchagua,” alisema rais Magufuli.
“Mmeona tuna kazi kubwa, bado tuna watoto wengi. Tuendelee kuwavumilia, nadhani na watanzania wameona,” aliongeza.
Aliwataka
wabunge wote kusimama pamoja bila kujali itikadi zao za vyama na
kuwasisitiza kuwa wanapaswa kuhakikisha kuwa Bunge la 11 linakuwa bunge
la kihistoria na kuacha masuala ya kupigana vijembe, kuzomeana na kutoka
nje.
Kwa
upande wake Spika wa Bunge hilo, Job Ndugai alimuomba radhi rais
Magufuli na Shein kwa kile kilichoanywa na wabunge wa Ukawa huku
akiahidi kuwa hali hiyo haitajirudia tena.
Ndugai
aliwaonya wabunge kuwa kitendo kilichofanywa ni cha aibu hivyo
hatawavumilia tena na kwamba wabunge wanaweza kumfanya akawa Spika mpole
ama kumfanya awe Spika ‘mbabe’.
“Mnaweza
kunifanya nikawa Spika mbabe sana… leo iwe mwisho. Ni kwa sababu wazee
hawa walikuwepo. Lakini wazee hao wasipokuwepo, wakifanya tena tabia
hii, basi… nisiseme sana,” alisema.
0 comments:
Post a Comment