Home » » Ni marufuku kuuza viwanja Kinondoni..mengine kutoka kwa DC Paul Makonda!!

Ni marufuku kuuza viwanja Kinondoni..mengine kutoka kwa DC Paul Makonda!!

Kufuatia migogoro ya muda mrefu ya ardhi katika kata za ya Wazo, Mabwepande pamoja na Bunju imekuwa ikiwaathiri wananchi zaidi ya laki 3 wanaoishi katika maeneo hayo.
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Paul Makonda leo ametolea ufafanuzi wa migogoro hiyo na kuamua kutafuta muafaka wa migogoro hiyo.
“Niligundua lazima nitafute mkakati mbadala wa kutatua changamoto hiyo, kumekuwa na kesi zaidi ya laki 3 na hata watu wa Manispaa wakitaka kwenda kule kutafuta muafaka wanaishia kupigwa, niliamua kuchukua hatua kwa kwenda kuwaona wananchi kwa kupitaa mtaa baada ya mtaa, nikalazimika kuunda kamati ya usuluhishi na kujipatia wajumbe zaidi ya 12 kwa kila mtaa” Paul Makonda.
“Tunayo kila sababu ya kutafuta majibu ili wananchi waweze kuwa na haki na kuishi kwa amani na kuendeleza makazi waliyo nayo, zipo hatua za kukubaliana kati ya wamiliki halali na wasio halali waliyokwenda kujenga katika hayo maeneo, tukiacha maeneo kwa muda mrefu hupelekea watu kuamini ni maeneo ya wazi na kuvamia viwanja vya watu wengine na kusababisha mgogoro”….
“Nimeelekeza kuanzia wiki ijayo watu kwenda kuyatambua maeneo kwa wale wanaodai ni maeneo yao, kama walipewa na Serikali ya kijiji au ni ya kwao binafsi, kuna watu wanauza maeneo ambayo si yao na anayeuziwa naye anauza..kwa sasa nimepiga marufuku biashara ya ardhi katika kata zote tatu  hadi pale watakapopatiwa umiliki, na mtu yoyote asiende kununua maeneo hayo kwa sasa”..Makonda.
Katika mkakati wa kufanya haya maeneo kuwa miji mikubwa amesema “Hadi pale Manispaa itakaporidhika haya maeneo yanamilikiwa na nani kwa kupata haki ya umiliki ndipo Manispaa itafanya nao maongezi ili kuwalipa fidia na kuyachukua maeneo hayo”
Facebook Blogger Plugin: Bloggerized by Joseph Kipangula Enhanced by Joseph Kipangula

0 comments:

Post a Comment

NURU FM 93.5 IRINGA

.

.

.

Nyali

Pages

Pages

Powered by Blogger.

Blog Archive

Search This Blog