Watu wawili wamefariki dunia katika
matukio mawili tofauti likiwemo la mtu mmoja mkazi wa mtwivila kuuawa kwa kuchomwa
na kitu chenye ncha kali shingoni na watu wasiojulkana manispaa ya iringa.
Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo
kamanda wa polisi mkoa wa iringa RPC RAMANDANI ATHUMANI MUNGI amesema kuwa
tukio hilo limetokea katika eneo la TRM Minyarani kata ya mkimbizi.
Katika tukio la pili kamanda MUNGI
ameongeza kuwa mtu mmoja amefariki dunia katika ajali baada ya kugongwa na pikipiki
eneo la mnazi mmoja kata ya Kitwiru.
Awali kamanda mungi ameongeza kuwa
jeshi la polisi linaendelea na uchunguzi
ili kuwakamata waliohusika kufanya mauaji ya JEOPHREY HARDSON.
0 comments:
Post a Comment