Wabunge wa vyama vya upinzani vinavyounda Ukawa wameonywa kutofanya jambo lolote litakaloashiria kuvuruga Bunge wakati Rais John Magufuli atakapolihutubia leo jioni.
Akiongea
jana mjini Dodoma, Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM ambaye pia ni
Mbunge wa jimbo la Mtama, Nape Nnauye alisema kuwa Wabunge hao wa Ukawa
wanapaswa kufahamu kuwa kitendo chochote watakachofanya kwa lengo la
kuvuruga hotuba hiyo ni kinyume cha sheria na taratibu za Bunge na
kwamba hawatavumiliwa.
Nape
alionesha kuwashangaa wabunge hao kudai kuwa hawamtambui Rais Magufuli
ili hali wanashiriki katika shughuli zote za Bunge ikiwa ni pamoja na
kumpigia kura Waziri Mkuu ambaye ameteuliwa na Rais huyohuyo wanaedai
hawamtambui.
Naye
Mbunge wa jimbo la Nzega, Dkt Khamis Kigwangala alisema kuwa wabunge wa
Ukawa wana haki ya kuingia Bungeni na kukaa kwa utulivu au kutoka nje
endapo hawatakuwa tayari kusikiliza hotuba hiyo lakini sio kuvuruga hali
ya amani ili watanzania wasipate nafasi ya kumsikiliza Rais.
“Hawawezi kuwanyima haki watanzania kumsikiliza Rais wetu akiwa anatoa dira ya uelekeo wa Taifa letu,” alisema Khamis Kingwangala.
Walisisisitiza kuwa watafanya ‘jambo’ ambalo hata hivyo hawakulitaja. Wabunge hao pia walisema kuwa wamemuandikiabarua Spika wa Bunge kuhoji uhalali wa hotuba ya Rais wakati Zanzibar bado haijampata Rais mpya
0 comments:
Post a Comment