Mradi wa mabasi yaendayo kasi Dar es
Salaam DART uko katika hatua za mwisho kukamilika na kuanza kutumika
kama moja ya njia za kurahisisha usafiri katikati ya Jiji.
Nimempata Kaimu Meneja msimamizi wa miundombinu mradi wa DART, Mohamed Kuganda… haya ni maneno yake ya kwanza kuhusu mradi huo >>> “Kwa
upande wa uharibifu wa miundombunu umekuwa ukitokea mara kwa mara na
hauwezi kuzuilika ikiwemo madereva kugonga nguzo za taa za barabarani
kutokana na kutumiwa wakati zikiwa katika ujenzi…”
Gharama za matengenezo ikitokea uharibifu huo zinamhusu nani >>> “Uharibifu
ukitokea wakandarasi wanarekebisha kwa kuwa mradi uko chini yao lakini
ikiwa tayari wamekabidhi, ni jukumu la TANROADS kufanya marekebisho“>>> Mohamed Kuganda.
Kwenye sentensi nyingine Mohamed Kuganda ana haya >>> “Ieleweke
kwamba dereva akifanya uzembe kwa kugonga taa za barabarani ni wajibu
wake kulipa na atashtakiwa kwa kosa la uharibifu wa mali za umma“.
Kuna suala la nauli pia mabasi ya mwendokasi yakianza safari, majibu yake ni haya >>> “Upande
wa nauli mpaka sasa mchakato bado haujakamilika kwa kuwa ni mrefu na
kwa sasa wadau wanafanya vikao kujadili, mchakato ukikamilika wananchi
watafahamishwa“>>> Mohamed Kuganda.
Unaweza kutazama hii video hapa chini…
0 comments:
Post a Comment