Leo mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Paul Makonda amekutana na viongozi mbalimbali ndani ya Wilaya yake na kuzungumzia mambo mbalimbali ya maendeleo ndani ya Wilaya hiyo.
Kikubwa alichozungumzia ni malalamiko kutoka katika idara mbalimbali ikiwemo ya ardhi, biashara katika maeneo yasiyo rasmi, mapungufu katika ofisi ya TAKUKURU pamoja na suala zima la ugonjwa wa Kipindupindu.
Kuhusu suala la usafi katika Manispaa ya Kinondoni..“Idara zetu hazifanyi kazi inavyopaswa, agizo la Rais kufanya usafi kwetu ni aibu ilipaswa tuanze kujiongoza wenyewe, mifumo yetu ya maji taka haijulikani,afisa biashara na watendaji wake kila mtu anafanya biashara kinyume na utaratibu, watu wanapika vyakula barabarani..alafu tukikaa ofisini tunajigamba tunaongoza kwa usafi” Paul Makonda.
“Tumefikia hatua tunasubiri kauli ya Rais ili kufanya usafi, ni aibu mtu mzima kuwa na jukumu lako alafu unaelekezwa na mtu mwingine kwenye idara yake…Asilimia 80 ya kushindwa kwa Serikali iliyopita sisi tumechangia, wananchi hawapati nafasi ya kukutana na viongozi wa juu lakini kwa wale viongozi wa chini ni rais lakini hawapati uShirikiano wowote kutoka kwao”...
Migogoro ya ardhi..“Mtendaji wa kata anashirikiana na watu kuuza ardhi za wananchi..hizi kesi za ardhi haziwezi kuisha kama tumefikia hatua ya kuwa wadanganyifu sisi viongozi wenyewe”…
Kukithiri kwa rushwa TAKUKURU haionyeshi utendaji wake wa kazi…“Takukuru ni moja ya ofisi ambayo nilitamani ifutwe, na hata ukimuuliza mwananchi wa kawaida atakwambia futa TAKUKURU, utendaji wao wa kazi hauonekani, rushwa imetawala kila mahali na hakuna wanachofanya lakini bado ni chombo kinachoheshimika sana…Ni moja ya chombo kinachotia aibu sana kwenye Taifa letu.
Kuhusu Hotuba ya Rais Je? ..”Moja ya mambo ya msingi aliyoyasema Rais wakati wa kampeni amekutana na malalamiko mengi uu ya rushwa na akafafanua ni jinsi gani inapoteza haki, Waziri mkuu naye aligusia ilo, sasa tujiulize kwa nini Rais kaona mambo ya rushwa ayaweke namba moja”.
0 comments:
Post a Comment