Kulikuwa na stori zikichukua nafasi kila siku kwenye vyombo vya habari kuhusu ishu ya viongozi na wanachama wa CHADEMA kuzuiwa kuaga mwili wa aliyekuwa Mwenyekiti wa Chama hicho Geita, Alphonce Mawazo.
Taarifa iliyotolewa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Charles Mkumbo
siku chache zilizopita iliagiza kwamba kusiwepo shughuli za kuaga mwili
wa marehemu huyo kutokana na ishu ya kipindupindu kilichoibuka maeneo
mbalimbali ikiwemo ndani ya Mwanza yenyewe.
Viongozi mbalimbali wa CHADEMA ikiwemo Mbunge na Mwenyekiti wa Chama hicho, Freeman Mbowe na Mwanasheria wa Chama hicho, John Mallya wamefika Mahakama Kuu Mwanza na kesi tayari imesomwa.
Sentensi za Mwanasheria wa CHADEMA, John Mallya hizi hapa baada ya kutoka nje ya Mahakama >>> “Leo
tumefungua kesi ya madai Mahakama kuu kwa hati ya dharura, mlalamikaji
wa kesi ni baba mdogo wa marehemu Mawazo… Maombi yetu ni kupata ruhusa
ya Mahakama ili kutengua zuio la Mkuu wa Polisi Mwanza kuhusu kuaga mwili wa marehemu Mawazo.”- John Mallya, Mwanasheria wa CHADEMA.
Sentensi nyingine za John Mallya ana haya >>> “Kuna Mawakili watatu, kesi imesikilizwa leo upande mmoja na upande wa pili wa RPC Mwanza na Mwanasheria wa Serikali
watasikilizwa kesho asubuhi… Jaji ameona jambo hili ni la dharura na
linahusu mwili wa mtu aliyekaa mochwari kwa zaidi ya siku nane, amesema
ataifanya kwa haraka.”-
Kuhusu mwendelezo wa kesi hiyo, Mahakama itaendelea nayo kesho Jumanne November 23 2015 na hiki ndio alichokisema Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe >> “Tumefungua
madai ya kutaka kumuaga Kamanda wetu Mawazo, madai yetu yamepokelewa
Mahakama kuu, yamepangiwa Jaji na kesho asubuhi suala letu litaanza
kusikilizwa” >>>
0 comments:
Post a Comment