Home » » Hukumu ya kesi ya Sheikh Ponda yaahirishwa Tena

Hukumu ya kesi ya Sheikh Ponda yaahirishwa Tena

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Morogoro, kwa mara nyingine tena imeahirisha hukumu ya kesi ya jinai inayomkabili Kiongozi wa Taasisi na Jumuiya za Kiislamu nchini Sheikh Ponda Issa Ponda.
 
Kesi hiyo iliyotarajiwa kutolewa hukumu yake leo Jumatano na Hakimu Mkazi wa Mahakama hiyo, Mary Moyo imeahirishwa na mshtakiwa amerudishwa rumande baada ya hakimu husika kutokuwepo mahakamani hapo kwa madai kuwa amekwenda kwenye kozi fupi ya kushughulikia kesi za uchaguzi mjini Dodoma  ambapo  shauri hilo limelazimika kuahirishwa na Hakimu Mkazi, Erick Rwehumbiza hadi Novemba 30, mwaka huu itakapofikishwa tena mahakamani hapo.
 
Mshtakiwa huyo anakabiliwa na mashtaka mawili ikiwemo kutoa maneno yenye kuhimiza imani za dini na kushawishi watu kutenda kosa, mashtaka anayodaiwa kuyatenda Agosti 2013.
 
Upande wa mashtaka wa kesi hiyo unawakilishwa na Wakili wa Serikali Mwandamizi, Benard Kongola, Sunday Hyera na George Mbalasa, wakati upande wa Mshitakiwa unawakilishwa na Wakili Juma Nasoro, Abubakar Salim na Bartholomeo Tarimo.
 
Awali hukumu ya Sheikh Ponda ilipangwa kutolewa  tarehe 19 mwezi  10 kabla ya kuahirishwa tena na shauri hilo kupangwa kutolewa hukumu Novemba 18 mwaka huu, kabla ya kuahirishwa tena hii leo hadi Novemba 30
Facebook Blogger Plugin: Bloggerized by Joseph Kipangula Enhanced by Joseph Kipangula

0 comments:

Post a Comment

NURU FM 93.5 IRINGA

.

.

.

Nyali

Pages

Pages

Powered by Blogger.

Blog Archive

Search This Blog