Mtu wangu wa nguvu November 28 zilipigwa mechi kadhaa kali barani Ulaya ila kwa upande wa Ligi Kuu Hispania mchezo wa kwanza kupigwa November 28 ulikuwa ni mchezo wa FC Barcelona ambao walishuka katika dimbani lao na Nou Camp kuikaribisha Real Sociedad iliyokuwa nafasi ya 14 katika msimamo wa Ligi Kuu Hispania (LALIGA).
Kama ilivyo kawaida yao FC Barcelona waliendelea kuutawala mchezo kwa asilimia kubwa kuzidi Real Sociedad ambao hadi dakika ya 70 walikuwa wana wastani wa asilimia 49 ya kumiliki mpira. FC Barcelona walianza kwa mashambulizi kwani dakika ya 13 Andre Iniesta alipiga kichwa kikagonga mwamba.
Mambo yalianza kuwa mabaya kwa upande wa Real Sociedad baada ya Dani Alves kutoa pasi ya goli na Neymar kupachika goli la kwanza kwa FC Barcelona dakika ya 22, dakika nne kabla ya kwenda mapumziko Dani Alves alitoa pasi ya pili ya goli na Luis Suarez kuiandikia FC Barcelona goli la pili dakika ya 41.
Mchezo uliendelea kuwa mgumu kwa Real Sociedad licha ya kuwa kipindi cha pili waliimarika kiasi na kujitahidi kumiliki mpira kidogo, Neymar dakika ya 53 akapachika goli la tatu na Lionel Messi akaitimisha kwa kufunga goli la nne dakika ya 90 na kufanya mchezo kumalizika kwa ushindi wa goli 4-0 dhidi ya Real Sociedad. Huu ni mchezo wa pili FC Barcelona kufunga goli 4-0 baada ya weekend iliyopita kumfunga Real Madrid.
Video ya magoli ya FC Barcelona
0 comments:
Post a Comment