Hizi haziwezi kuwa taarifa njema kwa mshambuliaji wa kimataifa wa Uingereza anayeichezea klabu ya Liverpool Daniel Sturridge ambaye hakupata nafasi ya kucheza wala kukaa benchi katika mchezo wa michuano ya UEFA Europa League usiku wa November 26 dhidi ya Bordeaux katika uwanja wao wa nyumbani wa Anfield.
Staa huyo wa Liverpool
ambaye alikuwa nje ya uwanja toka October 4 baada ya kuwa majeruhi na
kulazimika kuwa nje ya kwa muda, alikuwa akitazamiwa kucheza mchezo wa Europa League usiku wa November 26 ila stori mpya ni kuwa nyota huyo ameshindwa kurejea uwanjani baada ya kuonekana bado alikuwa na tatizo.
Daniel Sturridge
mwenye umri wa miaka 26 ambaye alikuwa akilalamika kuhisi maumivu
katika mguu wake, amepata nafasi ya kucheza mechi tatu pekee msimu huu
na 18 kwa mwaka 2015, alifunga magoli mawili katika ushindi wa magoli
3-2 dhidi ya Aston Villa September 26 lakini bado hajapata nafasi ya kucheza chini ya kocha mpya Jurgen Klopp
0 comments:
Post a Comment