Maisha yanabadilika kila siku, zamani
ilikuwa ukikutana na chupa au makopo ya maji au juice unayaona takataka…
sasahivi ni dili na watu wameweka nguvu zao kabisa kukusanya makopo na
kuyauza !!
Nigeria wamefanya kitu kingine zaidi mtu wangu, umewahi kuona nyumba za makopo??!!
Nigeria wamefanya kitu hicho, wamejenga nyumba kwa makopo ambapo ndani
ya makopo hayo kumejazwa mchanga halafu makopo yanapangwa vizuri kabisa
mpaka inakuwa nyumba ya kuishi.
Sifa nyingine kubwa za hizi nyumba ni kwamba zina uwezo wa kuzuia risasi na pia zinaweza kuzuia moto.
Unaweza kuwa na swali kwamba chupa kiasi
gani au chupa ngapi zinatosha kukamilisha mjengo??!! Jibu lake ni hili
hapa, kama unahitaji nyumba ya vyumba viwili inatakiwa kuwepo na chupa
14,000… Umevutiwa na ujenzi wa aina hii mtu wangu ???
0 comments:
Post a Comment