Na. Julius Mtatiro,
Mtatiro J.
Nilipo-
post juu ya jambo hilo mjadala mkubwa wa wananchi umekuwa ni kutaka
kujua sheria inaelekeza nini kwa mamlaka ya wakuu wa wilaya. Kwa uelewa
wangu wa shahada ya kwanza ya sheria nimeona niwawekee hapa ufafanuzi wa
kisheria kwa ajili ya faida yenu na mjadala mwingine tena.
SHERIA INASEMAJE?
Sheria
ya Tawala za Mikoa ya mwaka 1997 (The Regional Administration Act)
kwenye kifungu cha 15 (1) imeweka sharti muhimu kwa Mkuu wa Wilaya ikiwa
atahitaji kutumia mamlaka ya kuamrisha mtu akamatwe, kifungu hicho
kinamtaka afanye hivyo pale tu ambapo atakuwa amejihakikishia kuwa kosa
lililotendwa na mhusika athari yake huwa ni kukamatwa na kushtakiwa na
tena sheria imeweka masharti ya namna ya kushtaki.
JE KISHERIA DC MAKONDA ANA HAKI YA KUWAWEKA NDANI WATAALAM HAO?
Hapana,
kisheria hana mamlaka hayo, Kosa walilotenda watalaam hawa wa ardhi ni
la kuchelewa kwenye eneo la kazi, kosa la kuchelewa mahali kwenye
majukumu ya kawaida ya kupima ardhi haliwezi kamwe kumfanya mtu
ashitakiwe hadi pale ambapo kuchelewa huko kutakuwa kumesababisha
madhara makubwa na yanayoweza kuthibitishwa mahakamani.
Kwa hiyo kama Makonda amewaweka ndani anawajibika kwa mujibu wa sheria hii kuwapandisha kizimbani haraka kesho (Jambo ambalo atalikwepa kwani hawana kosa ambalo lina ?amount to being arrested and tried? yaani ?kukamatwa na kushtakiwa?).
Kwa hiyo kama Makonda amewaweka ndani anawajibika kwa mujibu wa sheria hii kuwapandisha kizimbani haraka kesho (Jambo ambalo atalikwepa kwani hawana kosa ambalo lina ?amount to being arrested and tried? yaani ?kukamatwa na kushtakiwa?).
JE, MAKONDA AKISHTAKIWA ANAWEZA KUPEWA ADHABU GANI?
Bahati
nzuri, sheria hiyohiyo katika kifungu cha 15 (1) imeeleza kuwa ikiwa
mkuu wa wilaya atatumia mamlaka yaliyowekwa na kifungu husika kwa maana
ya kutumia madaraka yake vibaya, atakuwa ametenda kosa na anaweza
kushtakiwa kwa mujibu wa kifungu cha 96 cha Sheria ya Kanuni ya Adhabu
(Penal Code).
Kifungu
hicho cha 96 (1) na (2) kinaeleza kuwa Mtu yeyote ambaye ameajiriwa
kwenye utumishi wa umma (akiwemo Mkuu wa Wilaya) anayetenda au kuamrisha
utendekaji wa jambo kwa kutumia vibaya madaraka ya kazi yake, kitendo
chochote cha dhuluma ambacho kinazuia haki ya mwingine atakuwa ametenda
kosa na akitiwa hatiani anaweza kufungwa miaka mitatu jela.
JE WATAALAM HAO WA ARDHI WANAWEZA KUMSHITAKI MAKONDA?
Ndiyo,
wataalam wa Ardhi waliotendewa amri hiyo wanaweza kumshitaki Paul
Makonda kwa kitendo chake cha kutumia vibaya madaraka yake lakini bahati
mbaya itakayowakuta ni kwamba Sheria hiyo hiyo ya Kanuni ya adhabu
kwenye kifungu cha 96 (3) imeweka sharti lingine kuwa Uendeshaji wa
shitaka kwa husika hautaanzishwa mpaka kitakapotolewa kibali cha
Mkurugenzi wa Mashitaka (Kesi ya Nyani amekabidhiwa ngedere).
Mtatiro J.
Upande wa Pili Wa Shilingi
Kwa nini mkuu wa wilaya aliamua kuwatia ndani? Wananchi wa eneo husika walikichukuliaje kitendo hicho??
0 comments:
Post a Comment