Ikitokea unakuwa sehemu ya watu walionusurika kwenye ajali, jambo kubwa ambalo wengi wanaanza nalo ni kumshukuru MUNGU kwa kutoka salama !!
Kama uko karibu na headlines za stori za kimataifa najua utakumbuka ile ajali ya ndege ya British Airways iliyotokea uwanja wa ndege Las Vegas Marekani wakati ndege ikijiandaa kupaa.
Taarifa nyingine toka Chicago Marekani inahusu kesi ambayo imefunguliwa kuzishtaki Kampuni mbili, GE Aviation watengenezaji wa engine ya ndege iliyopata ajali, pamoja na Boeing Company ambao ndio watengezaji wa ndege yenyewe.
Abiria hao 65 waliofungua kesi hiyo
wamesema wanazishtaki Kampuni hizo kwa sababu walipata misukosuko wakati
wa ajali hiyo ambayo ndege waliyopanda ililipuka na kushika moto kwenye
engine yake moja wakati ikiwa kwenye njia ya kurukia ndege uwanja wa McCarran International Airport, September 8 2015.
0 comments:
Post a Comment