Katibu wa Itikadi na Uenezi Nape Nnauye amesema jina la Ndugai limepitishwa na kamati ya wabunge wote baada ya wenzake wawili Tulia Ackson na Abdullah Mwinyi kujitoa.
Kingine kilichotufikia leo kutoka Dodoma ni uteuzi wa Rais Dk. John Magufuli ambaye amemteua Dkt.Tulia Ackson Mwansasu kuwa Mbunge wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Jina la Mwansasu ambaye alikuwa mwanasheria mkuu msaidizi ni miongoni mwa majina matatu yaliyopitishwa jana na kamati kuu akiwemo Job Ndugai pamoja na Abdullah Mwinyi kuwania nafsi ya kiti cha spika ambapo leo Ndugai ametangazwa kuwania kiti hicho.
Katibu wa Bunge Dkt.Thomas Kashillilah amethibitisha uteuzi huo ambao kwa mujibu wa katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ibara ya 66 (e) inampa Rais madaraka kuteua wabunge wasiozidi kumi.
0 comments:
Post a Comment