Moja ya stori kubwa niliyokutana nayo
leo ni hii ambayo imeripotiwa kwenye habari Kituo cha ITV ambayo inahusu
taarifa kutoka wilaya ya Kahama mkoa wa Shinyanga… kilichoipa uzito
zaidi hii taarifa ni ishu ya watu watano kati ya sita waliokuwa
wamefukiwa na kifusi katika machimbo ya Nyangarata kwa siku 41,
wameokolewa wakiwa hai.
Watu hao walifukiwa wakiwa kwenye
harakati za kuokoa wenzao waliokuwa wamenasa kwa kufukiwa na kifusi, hii
ni sehemu ya kilichosemwa na mmoja wa watu ambao walifukiwa na wametoka
hai >>> “tulikuwa tumebaki
watu sita chini, tukawa tunakunywa maji tuliyoyakanyaga na kuyakojolea,
tulikula magome ya miti, mende pamoja na vyura” >>> Joseph Burure.
Wenyeji wa eneo hilo wamesema walikuwa
kwenye jitihada za kuitoa miili ya watu hao kutoka ndani ya machimbo
ambapo walihisi kwamba wamefariki, ila baadae wakagundua kwamba kuna
watu walionasa chini, ikabidi waanze taratibu za kuwatoa, wakawakuta
wakiwa hai huku wakiwa na upungufu mkubwa wa maji mwilini pamoja na
majeraha… mmoja kati ya watu hao alifariki, watano wakatoka hai.
0 comments:
Post a Comment